Trump aapa kuwa Rais wa 47 wa Marekani

Washngton. Donald Trump ameapishwa kuwa Rais wa 47 wa Marekani leo Jumatatu, Januari 20, 2025, katika sherehe rasmi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Capitol, Washington D.C.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na waalikwa mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa, wafuasi wake, na wawakilishi wa nchi mbalimbali.
Trump, ambaye alishinda kwa tiketi ya Chama cha Republican, alishinda uchaguzi wa Novemba 2024 dhidi ya mpinzani wake wa Chama cha Democratic, Kamala Haris na kurejea madarakani baada ya muhula wake wa kwanza wa 2017 hadi 2021.
Endelea kufuatilia Mwananchi