Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndege iliyobeba watumishi wa UN yapata ajali, yaua mmoja

Muktasari:

  • Ndege iliyokuwa imekodishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) imepata ajali ilipokuwa ikijaribu kuruka na kugonga jengo na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Somalia. Mtu mmoja amefariki dunia huku mwingine akipata majeraha mabaya kufuatia ajali ya ndege ya mizigo katika mji wa Elberde nchini Somalia.

Kwa mujibu wa tovuti ya Citizen, ndege hiyo aina ya Skyward Fokker 50 Tail (5Y- JWG), ambayo ilikuwa imekodishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), ilishindwa kupaa na kugonga jengo katikati mwa mji.

Ndege hiyo inayosimamiwa na Jetways inadaiwa ilikuwa imebeba uzito wa tani 7 wakati ilipopata ajali hiyo.

Watu wanne ndio waliripotiwa kuwemo ndani ya ndege na wawili kati yao wamethibitishwa kuwa wako salama.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Somalia (SCAA) imethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ikisema uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo.

"Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Somalia inapenda kuthibitisha kuwa ndege aina ya Fokker 50 (F50) Cargo inayosimamiwa na Jetways, ilianguka kwenye njia ya kurukia ndege katika Uwanja wa Ndege wa Ceel leo (jana) Januari 18, 2024 saa 11:30 asubuhi (saa za ndani)," imesema taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo.

"Ndege hiyo ilikuwa na jumla ya wafanyakazi wanne, kuna kifo kimoja, na majeruhi mmoja,” imeongeza taarifa hiyo.