Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muhoozi: Hakuna wa kunipiga marufuku kwa chochote

Muktasari:

  • Jenerali Muhokozi amezungumza hayo baada ya kauli ya baba yake, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni aliyoitoa Jumapili iliyopita katika mahojiano yaliyorushwa na KTN ya Kenya, akisema kuwa mwaneye atakaa kando kwenye mtandao wa Twitter linapokuja suala la mijadala ya mambo ya Serikali.

Uganda. Siku chache baada ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kusema kuwa mtoto wake, Muhoozi Kainerugaba atakaa kando kwenye mtandao wa Twitter linapokuja suala la mijadala ya mambo ya Serikali, mwenyewe amesema hakuna wa kumzuia.

 Jumapili iliyopita katika mahojiano yaliyorushwa na KTN ya Kenya, Rais Museveni alisema, "Ataondoka Twitter. Twitter sio tatizo, tatizo ni kile unachoandika. Kuzungumza kuhusu nchi nyingine na siasa za upendeleo za Uganda ni jambo ambalo hapaswi kufanya na hatalifanya."

Jana Jumanne Oktoba 18, 2022 katika mtandao huo, Jenerali Muhokozi amesema kuwa yeye ni mtu mzima na hakuna wa kumpiga marufuku kwa kitu chochote.

“Namesikia mwanahabari kutoka Kenya akimuuliza babaangu anipige marufuku kwenye kwa Twitter? Je, huo ni utani? Mimi ni mtu mzima na hakuna mtu atakayenipiga marufuku kwa kitu chochote” ameandika

Jenerali Muhokozi amekuwa akiibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu maandiko yenye utata anayoposti kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter.

Miongoni mwa andiko lake lililozua mijadala ni pamoja na la kumlaumu Rais mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kutogombea muhula wa tatu wa uongozi wa nchi hiyo hali iliyosababisha baba yake kuingilia kati.

Oktoba 5 mwaka huu, Rais Museveni aliwaomba radhi wananchi wa Kenya kutokana na andiko lililochapishwa na Jenerali Muhokozi la kumlaumu Rais mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kutogombea muhula wa tatu wa uongozi wa nchi hiyo.

Kupitia ujumbe wake aliouchapisha katika mtandao wa kijamii Jenerali Kainerugamba aliandika;

“Shinda yangu pekee na kaka yangu mkubwa ni kwamba hakugombea muhula wa tatu. Tungeshinda kwa urahisi,” ulisomeka sehemu ya ujumbe huo.

Ingawa Kainerugaba amekanusha mara kwa mara madai kwamba ana nia ya kumrithi baba yake mwenye umri wa miaka 78 lakini baadhi ya maandiko yake yanaonyesha kuwa na nia hiyo.

Oktoba 15 mwaka huu Kainerugaba aliandika kwenye Twitter akiwaambia wapinzani kuwa baada ya baba yake, atawashinda katika uchaguzi kwa kuwa Waganda wanampenda kuliko wanavyopenda upinzani.

“Kwa wapinzani wa Uganda, baada ya baba yangu, nitawashinda vibaya katika uchaguzi wowote. Waganda wananipenda kuliko walivyowahi kuwapenda ninyi,” aliandika.