Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marekani yatoa msaada wa kijeshi Ukraine

Muktasari:

  • Msaada huo mpya wa kijeshi kwa Ukraine unaotokana na hifadhi zilizopo za silaha, unajumuisha mizinga, mifumo ya ulinzi wa anga na ya roketi za masafa marefu.

Dar es Salaam. Waziri wa ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, ametangaza msaada mpya wa kijeshi wa Dola milioni 100, takribani Sh250 bilioni kwa Ukraine.

Mtandao wa Voa umeripoti kuwa waziri huyo ametangaza msaada huo katika ziara ya kimyakimya aliyoifanya Kyiv jana, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwahakikishia viongozi wa Ukraine kwamba Marekani itaendelea kuunga mkono mapambano ya nchi hiyo dhidi ya kile alichokiita “uvamizi wa Russia.”

Taarifa ya VOA inasema kuwa baada ya safari ya treni ya usiku kutoka Poland, Waziri Austin, alikutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy mjini Kyiv, ambaye alimshukuru Austin kwa ziara hiyo.

Rais Zelenskyy amesema kwenda kwa waziri huyo ni ishara muhimu sana kwa Ukraine, na anaishukuru nchi hiyo kwa kuwa pamoja na Ukraine, katika vipindi vigumu miaka yote.

Msaada wa ziada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine unatokana na hifadhi zilizopo za silaha na unajumuisha mizinga, mifumo ya ulinzi wa anga na ya roketi za masafa marefu.

Kwa mujibu wa RFI, Alhamisi November 2, 2023; Baraza la Wawakilishi la Marekani, lilikuwa na kibarua kigumu baada ya kutokea mgawanyiko juu ya aina ya msaada wa kutoa kwa washirika wake nje ya nchi hiyo.

Wakati upande wa Democrats na Republicans wakitaka kupitishwa mara moja juu ya msaada wa kijeshi kwa Israeli, ambaye kimsingi ni mshirika wa muda mrefu wa Marekani katika vita na Hamas, hali ilikuwa ngumu kwa Ukraine.

Washington ndiyo mtoaji mkubwa zaidi wa misaada ya kijeshi kwa Kyiv, ikiwa imetoa mabilioni ya dola za Marekani tangu kuanza kwa mzozo wa Ukraine na Russia Februari mwaka jana.

Ukakasi huo wa maamuzi ulikuwa unaiweka rehani ahadi ya Rais wa marekani, Joe Biden ya kuendelea kuisaidia Ukraine kifedha, iliyosisitizwa tena wakati wa ziara ya Rais Zelensky mjini Washington Septemba.

Katika Bunge la Marekani, kuna upande mmoja wa Baraza la Wawakilishi, linalotawaliwa na wahafidhina na ambapo wabunge wa mrengo wa kulia wanatoa wito wa kukomeshwa mara moja kwa misaada kwa Kiev.

Kwa upande mwingine, kuna Baraza la Seneti, lenye wabunge wengi wa Democratic na wapinzani wao  Republican unapendelea zaidi misaada kwa Ukraine.

Akifahamu mgawanyiko miongoni mwa sehemu ya wanasiasa wa Marekani, Rais Biden aliamua kuchanganya ombi lake la msaada kwa Ukraine na lile la Israeli.