Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bodaboda 10 wafariki dunia ajali ya lori

Umati wa watu wakiwa kwenye eneo ilipotokea ajali katika Kaunti ya Migori nchini Kenya.

Muktasari:

  • Watu 10 wamefariki dunia baada ya ajali ya lori ambalo lilifeli breki na kuwagonga vijana wa bodaboda waliokuwa kijiweni wakisubiri abiria.

Kenya. Watu 10 wamepoteza maisha leo Jumamosi Aprili 8, 2023 katika Kaunti ya Migori nchini Kenya kutokana na ajali ya lori ambalo inaelezwa lilifeli breki na kuparamia kijiwe cha bodaboda.

 Watu hao waliopoteza maisha inaelezwa ni vijana wa bodaboda waliokuwa wakisubiria wateja kwenye kijiwe chao.

Taarifa ya awali kupitia mtandao wa Tuko nchini Kenya imeeleza kuwa lori hilo la kubeba mchanga, lilipoteza mwelekeo na kugonga kundi la bodaboda ambao walikuwa pembezoni mwa barabara wakisubiri abiria.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema muda mfupi eneo hilo lilitapakaa damu na miili ya watu ambapo juhudi za kuwaokoa waliopata majeraja zilikuwa zinaendelea.

“Miili yenye damu imesambaa katika eneo hilo na vyuma vinaonekana vimetapakaa damu,” ameeleza mmoja wa shududa ambaye hatutaka kutaja jina lake.

Umati mkubwa wa watu umemiminika eneo la tukio ili kuwanusuru majeruhi na kuwawahisha hospitalini kwa matibabu na wengine wakijaribu kuwatambua ndugu zao.

Shududa mwingine aliyezungumza na kituo cha runinga ya TV47, amesema breki za lori hilo inaonekana zilifeli na gari hilo kuingia katika kundi hilo la bodaboda ambao walikuwa wanasubiri abiria.

Ajali hiyo imetokea karibu na Shule ya Msingi ya Migori ambapo lilikuwa limejaa damu na miili kabla ya muda mfupi polisi kufika na kuwapeleka kuwahifadhi.

Kiongozi wa upinzani nchini humo, Raila Odinga ametoa pole kwa wafiwa ajali hiyo ilipolekea watu 10 kufariki dunia.