Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ang’atwa na kunyofolewa mdomo na mchepuko wake

Muktasari:

  • Inaelezwa kipigo kilivyozidi ndipo majirani wakasikia kelele na kwenda kumuokoa wakamkuta anabamizwa ukutani, wakamuokoa na kumpelekea hospitali.

Kakamega. Mkazi wa Kakamega, Douglas Shisia amejikuta  katika maumivu baada ya kung’atwa na kunyofolewa mdomo na mwanamke aliyetajwa kuwa ni mchepuko wake, alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake.

Shisia (45) ambaye anaishi Nairobi na familia yake akiwamo mkewe na watoto, alisafiri hadi Shiatsala Kakamega, anapoishi mchepuko huyo ambaye jina lake halikufahamika Jumatano Aprili 2, 2025 kwa lengo la kumtembelea. 

Alieleza kwamba alipofika kwa mpenzi wake, mambo yalibadilika baada ya kuzuka ugomvi kati yao, kwani alimjeruhi kwa kumng'ata mdomo wa chini kisha kumpiga.

"Tumekuwa na uhusiano kwa muda na tulikutana mara moja mwaka jana, kumekuwa na hali ya kutoelewana kutokana na hali ya kutoaminiana,” amesema.

“Nilikuja ili tutatue changamoto kati yetu, lakini aliamua kunipiga na kuniacha na majeraha," amesema Shisia alipozungumza na chombo cha habari cha Tuko News cha Kenya.

Inaelezwa kipigo kilivyozidi ndipo majirani walikwenda na kumuokoa, hata hivyo wakalikuta amejeruhiwa na waliamua kumpeleka Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Manyala.

Tukio hilo liliripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Manyala, na Shisia anasubiri hatua zaidi za kipolisi dhidi ya  mwanamke huyo.

“Nimesharipoti polisi na kupewa namba ya OB, pia daktari amesaini fomu ya P3 ili nipate haki,” amesema.

Daktari mkuu katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Manyala, Butere Japhet amethibitisha tukio hilo, akieleza kuwa walimuhudumia na kumpatia matibabu eneo la mdomoni alipokuwa amejeruhiwa zaidi.