Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anayedaiwa kuwa wakili ‘feki’ aelezea njia alizopita hadi kutoboa

Muktasari:

  • Brian Mwenda, anayedaiwa kuwa wakili ‘feki’ ambaye mamlaka nchini Kenya zinamshikilia akituhumiwa kujitambulisha na kufanya kazi ya uwakili bila kuwa vigezo vinavyotamkwa kwenye sheria za nchi hiyo, ameelezea maisha yake.

Dar es Salaam. Brian Mwenda, anayedaiwa kuwa wakili ‘feki’ ambaye mamlaka nchini Kenya zinamshikilia akituhumiwa kujitambulisha na kufanya kazi ya uwakili bila kuwa vigezo vinavyotamkwa kwenye sheria za nchi hiyo, aamua kufunguka na kuelezea maisha yake.

 Mwenda amefanya hivyo katika akaunti yake katika mtandao wa X (zamanani Twitter) ambapo ameeleza kuwa hadidhi yake ilianza katika Shule ya Msingi Madaraka, aliposoma darasa la 1 hadi 8.

Mwenda anadai Jiji la Nairobi ni kama Mji Mkuu wa Afrika, wenye maeneo ya kifahari, vitongoji maridadi, hata hivyo imekuwa ni changamoto kubwa zaidi kwake kuishi katika Jiji hilo.

Kwa mujibu wa chapisho hilo, Mwenda alipomaliza elimu ya msingi, alifaulu kwa alama za wastani ambazo zingemwezesha kupata shule bora ya sekondari huku akisema “Nilijua kuwa nimeifelisha familia yangu yote, lakini nilikuwa na ndoto.”

Anaendelea kuelezea kisa chake kuwa aliamua kujiunga na moja ya shule licha ya wazazi wake kutokuwa na uwezo na kwamba maisha hayakuwa mazuri.

Katika kipindi cha mpito kutoka kuandika abcd hadi kiwango cha ujengaji wa hoja hasa kutokana na maswali, ulimshitua na ilibidi azoee hali hiyo, kwani alijua kuwa kwenda kwake shule kulikuwa ni kujiepusha na matumizi ya dawa ya kulevya na ushawishi mbaya kutoka kwa wenzake katika Mtaa wa Kawangware.

“Ilibidi maisha yasogee kwa kuwa nilizoea na niliweza kujikuta katika nafasi ya 20-30 kati ya wanafunzi wenzangu 120, nafasi hiyo kwangu ilinitosha kwa sababu sikuwa na uwezo mkubwa sana, lakini Joseph Murphy alisema "sheria ya maisha ni sheria ya imani.,”

“Ilikuwa ni mitihani baada ya mitihani, miaka minne baadaye kijana mdogo wa Kawangware alimaliza elimu yake ya sekondari (KCSE),” ameeleza Mwenda katika chapisho lake na kuongeza;

“Ilikuwa 2016, matokeo ya KCSE yakitolewa, yakithibitisha kuwa kijana mdogo ameupiga mwingi, nilipomuelezea baba yangu habari hizo kwa mara ya kwanza, hakuamini, alishangaa sana. Ni alama hii ya B+ inayokupeleka moja kwa moja hadi chuo, sivyo? Aliniuliza na mimi kumjibu ndiyo.”

“Muda ukaenda haraka na 2017, ndoto yangu ya kujiunga na chuo ilitimia nilipoitwa kujiunga na Chuo Kikuu maarufu nchini Kenya, chenye viwango vya kimataifa, ukiniuliza ni Chuo Kikuu cha Chuka, nikisomea Shahada ya kwanza ya masomo ya kuchunguza uhalifu,”

Kwa mujibu wa Mwenda ameahidi ataendelea kuelezea kisa cha maisha yake.