Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh395 milioni zakopeshwa kwa vikundi 44 Ileje

Mkuu wa wilaya ya Ileje Mkoani Songwe, Farida Mgomi (wa nne mbele kutoka kushoto) akiwa ameshika hundi ya fedha na kukabidhi kwa kikundi cha wanawake walionufaika na mkopo huo .Picha na Denis Sinkonde

Muktasari:

  • Koimani amesema fedha hizo zilizotolewa kati yake Sh269 milioni zimetokana na marejesho kutoka kwenye vikundi vilivyokopeshwa awali, na fedha Sh126 milioni ni asilimia 10 kutokana na mapato ya ndani.

Ileje. Halmashauri ya Ileje Mkoani Songwe imetoa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi 44 vya vijana wanawake na wenye ulemavu yenye thamani ya Sh395.2 milioni ambayo hutolewa bila riba kwa mujibu wa sheria za serikali za mitaa sura 290 kifungu 37 (a).

Akisoma taarifa ya utoaji wa mikopo hiyo ya robo ya pili ya mwaka 2026 afisa maendeleo ya jamii na  mratibu wa mikopo wilayani humo Romana Koimani amesema vikundi 20 vya vijana vimekopeshwa Sh232.6 milioni, vikundi 22 vya wanawake vimekopeshwa Sh161 milioni na vikundi 2 vya watu wenye ulemavu vimekopeshwa Sh1.6 milioni.

Koimani amesema fedha hizo zilizotolewa kati yake Sh269 milioni zimetokana na marejesho kutoka kwenye vikundi vilivyokopeshwa awali, na fedha Sh126 milioni ni asilimia 10 kutokana na mapato ya ndani.

“Licha ya kutoa mikopo hiyo bado tunakabiliwa na changamoto ya baadhi ya wanavikundi kutokuwa na uhalisia wa andiko la mradi wa fedha ya mikopo inayoombwa kwa baadhi ya vikundi na   uwepo wa maombi mengi ambayo inapelekea halmashauri kushindwa kutoa mikopo kwa wakati kwa vikundi vyote,” amesema Koimani. 

Aidha amesema halmashauri hiyo imetoa mikopo kwa mwaka wa fedha   2024/2025 Sh711.2 milioni, ambapo vikundi vya wanawake 53  vilipata Sh387 milioni , vikundi 35 vya vijana vilipata Sh321 milioni  na kikundi kimoja cha mwenye ulemavu aliyepata Sh3 milioni.

“Mwaka 2025/ 2026 walitoa mikopo yenye jumla ya Sh760.2 milioni ambapo vikundi vya wanawake 53 vimepata Sh349 milioni, vijana vikundi 41 vimepata shilingi 406.6 na vikundi 3 vya watu wenye umelavu vimepata mkopo wa Sh4.6 milioni,” amefafanua Koimani.

Vicente soko mkazi wa Itumba mnufaika wa mikopo hiyo ameishukuru serikali kwa kuwanufaisha vijana kuwapa mikopo isiyo na riba kwani itawarahisishia kufanya kazi kwa weledi kwani awali walikuwa hawana utoshelevu wa vitendea kazi ikiwepo Kopresa katika kituo chao cha kazi.

Harris Mboya mkazi wa kijiji cha Mlale amesema anayejishughulisha na uuzaji wa nafaka amesema mkopo huo walioupata wa Sh6 milioni  watajitahidi kujikita kuwekeza kwenye mazao kama andiko lao linavyojieleza ili waweze kupata faida ya biashara ya mazao.

Akizungumza katika hafla hiyo, mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi amewahimiza wanufaika kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa pamoja na kuhakikisha wanairejesha kwa wakati ili kutoa nafasi kwa vikundi vingine kunufaika.

Mgomi amewasisitiza wanufaika wa mikopo hiyo kuwa nidhamu ya matumizi ya fedha na kujiepusha kitumia kama fimbo ya kunyanyasa familia zetu bali mjikite kufanya shughuli zilizoainishwa kwenye maandiko yenu kwani urejeshaji wa mikopo ni msingi wa uendelevu wa mpango huo.

"Niwatake wasimamizi wa mikopo hususani Maafisa Maendeleo kuwasaidia wanufaika kutumia ipasavyo mfumo wa Wezesha Portal unaotumika katika uombaji wa mikopo hiyo, ili kuhakikisha uwazi, ufanisi na upatikanaji wa taarifa sahihi kwa waombaji wote," amesema Mgomi.

Katika hatua nyingine, amewaasa wadau wa sekta mbalimbali kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuweka mazingira wezeshi pamoja na kutoa ushauri na msaada wa kitaalamu kwa wanufaika wa mikopo hiyo.