Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania hatarini kupoteza soko la korosho duniani

Zao la Korosho

Muktasari:

Ni baada ya kubainika kuwapo kwa vitendo vya kubadilisha madaraja ya korosho wakati wa kusafirisha.

Mtwara. Wakulima wa zao la korosho nchini wako hatarini kupoteza soko duniani kufuatia udanganyifu unaodaiwa kufanyika katika maghala ya kuhifadhi zao hilo wakati zikisubiri kusafirishwa kwenda nje.

Hali hiyo imesababisha zaidi ya tani 400 za korosho kukwama katika Bandari ya Dar es Salaam wakati zikisubiri kwenda nchini Vietnam, baada ya mnunuzi kupata wasiwasi na kuzifungua kisha kukuta zimeota, jambo ambalo limethibitishwa na Bodi ya Korosho. Mchezo huo mchafu hufanywa na baadhi ya watu wenye masilahi binafsi.

Hayo yalielezwa juzi katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mtwara (RCC), kilichoshirikisha wadau mbalimbali.

Akizungumza baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya kilimo, Mbunge wa Newala ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora, George Mkuchika aliitaka Bodi ya Korosho kutolea ufafanuzi juu ya malalamiko yaliyotolewa na Kampuni ya Export Trading iliyobambikiwa korosho zisizo na kiwango zikiwa ghalani zikisubiri kusafirishwa.

Akizungumzia hilo, Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho, Mfaume Juma alikiri kuwapo kwa malalamiko yaliyotolewa na kampuni hiyo, kuilazimu bodi hiyo kuitisha mkutano kujua ni kitu gani kilichosababisha korosho zilizothibitishwa kuwa daraja la kwanza kushuka kiwango.

Mbunge wa Mtwara Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia alisema kutotumika kwa Bandari ya Mtwara kunaweza kuwa moja ya sababu inayochangia korosho za mkoa huo kuonekana chafu wakati zimetoka katika mikoa mingine kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa kikao, Mkuu wa Mkoa, Halima Dendego alimtaka kila mmoja kutimiza wajibu wake kutokana na kilichotokea na wakulima kupatiwa haki zao.