Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Itakachokifanya Tanzania kukabili athari vita Mashariki ya kati

Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha 2026/27 Aprili 1, 2026 Bungeni Jijini Dodoma.

Muktasari:

  • Waziri Mkuu ametoa majibu hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kaskazini (ACT-Wazalendo) Ado Shaibu ambaye amehoji Serikali inachukua hatua gani kukabiliana na yatokanayo na vita hiyo.

Dodoma. Serikali ya Tanzania imetaja mambo mawili katika kukabiliana na athari zitakazojitokeza kutokana  na vita inayoendelea Mashariki ya Kati kwa lengo la kunusuru mtikisiko huo.

Mgogoro huo kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran umeanza kuathiri uzalishaji na usafirishaji wa mafuta ghafi duniani, hasa baada ya kufungwa kwa Mlango wa Hormuz ambao hupitisha takribani asilimia 20 ya mafuta yote yanayosafirishwa duniani.

Akijibu maswali ya papo kwa hapo bungeni leo Alhamisi Aprili 2, 2026, Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ametaja mambo hayo ni kuongeza nguvu katika shughuli za uchimbaji madini na kubana matumizi.

Waziri Mkuu ametoa majibu hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kaskazini (ACT-Wazalendo), Ado Shaibu ambaye amehoji Serikali inachukua hatua gani kukabiliana na athari zitokanazo na kuendelea kwa vita hiyo.

Shaibu amesema matokeo ya vita hivyo yatasababisha mtikisiko katika usafiri, shughuli za madini na kwenye masuala ya bima, hivyo akaomba kutambua mkakati wa Serikali kama imeshaanza kuchukua hatua za kubainisha.

Waziri Mkuu amesema, Tanzania siyo kisiwa kwani inafanya biashara kama ilivyo kwa mataifa mengine hivyo nayo ni miongoni mwa mataifa yatakayokumbwa na mtikisiko huo.

"Tanzania inafanya biashara na inategemeana na mataifa mengine hivyo tumeshafanya tathimini ya kutosha kujua athari hizo pamoja na ongezeko la bei kwa baadhi ya bidhaa lakini tutaendelea kujulishana wakati huu ambao wabunge tutakuwa hapa," amesema Dk Mwigulu.

Kwenye suala la uchimbaji madini, Waziri Mkuu amesema nguvu kubwa itawekwa huko kwani wanatambua sekta hiyo ni miongoni mwa maeneo ambayo ikisimamiwa vizuri inaweza kupunguza mtikisiko huo.

Dk Mwigulu amesema hata katika kipindi cha mwaka jana madini yalichochea kwa kiasi kikubwa mapato na hasa kupitia wachimbaji wadogo ambapo nchini kila wilaya inaelezwa kuwa na madini licha ya ukweli kuwa eneo lililofanyiwa utafiti ni asilimia 16 tu.

Waziri Mkuu amesema mkakati mwingine ni kubana matumizi ambapo lazima Serikali ifanye hivyo ili kuachana nayo katika maeneo ambayo hayana ulazima wa kufanya hivyo.

Katika hatua nyingine, Spika wa Bunge, Mussa Zungu ametangaza Kamati ya Nishati na Madini leo Alhamisi Aprili 2, inakutana kufanya kikao cha tathimini ya hali ya mafuta nchini kufuatia agizo alilolitoa jana.

Mapema jana Spika Zungu aliagiza Kamati hiyo kukutana na Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi ili wapeleke majibu na tangazo la leo wameomba wabunge wengine wanaopenda kuungana na kamati hiyo kufanya tathimini waende.