Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CAG: Sh1.14 trilioni zilizokusanywa na TRA hazikupelekwa panapohusika

Muktasari:

  • CAG anasema jambo hilo ni kinyume na Ibara ya 135(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoeleza kuwa fedha zilizotengwa kwa madhumuni maalumu hazipaswi kuingizwa katika Mfuko Mkuu wa Serikali.

Dar es Salaam. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeeleza kuwa Sh1.14 trilioni ya tozo mbalimbali kilichokusanywa kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hazikupelekwa katika taasisi husika.

CAG amesema kuwa katika ukaguzi wake kwa mwaka wa fedha 2023/24 ulibaini kuwa jumla ya Sh2.59 trilioni zilikusanywa na TRA kwa niaba ya Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), Wakala wa Nishati Vijijini (Rea), Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) na Mfuko wa Reli kisha kuhamishiwa Wizara ya Fedha.

Hata hivyo, Wizara ya Fedha ilihamisha Sh1.44 trilioni pekee kwenda mifuko hiyo husika, hivyo salio la Sh1.14 trilioni sawa na asilimia 44 ya jumla ya fedha zilizokusanywa, hazijapelekwa kwenye mifuko husika.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa kutowasilishwa kwa kiasi chote cha makusanyo ya tozo na ada za mafuta kumevunja matakwa ya Katiba na kudhoofisha uwezo wa mifuko na wakala kugharamia miradi ya maji, barabara, reli na umeme vijijini na hali hii imesababisha kuchelewa kwa maendeleo ya miundombinu na kupunguza ufanisi wa utekelezaji wa miradi.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 16,2025 Dodoma. Picha na Hamis Mniha

Amesema jambo hilo ni kinyume na Ibara ya135(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoeleza kuwa fedha zilizotengwa kwa madhumuni maalumu hazipaswi kuingizwa katika Mfuko Mkuu wa Serikali.

Pia kanuni za Petroli (Uwekaji wa Ada ya Petroli) za mwaka 2015, Kanuni za Mfuko wa Taifa wa Maji za mwaka 2019, Sheria ya Barabara na Ada za Mafuta, sura ya 220, na Sheria ya Reli, 2017, sura ya 170 zinaitaka TRA kukusanya ada na tozo za mafuta kwenye dizeli na petroli na kuziwasilisha kwenye akaunti husika za REA, NWF, Bodi RFB na RF.

 “Ninapendekeza kwamba Serikali ihakikishe uwasilishaji wa haraka na kamili wa ada/tozo za mafuta kwa mifuko maalumu ili kuwezesha ufadhili wa miradi ya maji, barabara, reli na umeme vijijini hapa nchini,” ameelekeza CAG katika ripoti hiyo.