Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zuchu arusha dongo ishu ya Mondi, Rita ajibu mapigo

Muktasari:

  • Hii ni baada ya video ya Zuchu kusambaa kwenye mitandao ya kijamii akiimba huku mistari ya wimbo ikiwa hivi, "Unagombana na mimi kwani ndio nilikunyima kodi?"

Dar es Salaam. Ni wazi kuwa kwenye mitandao ya kijamii kinachozungumzwa zaidi kwa sasa ni habari ya mwanamuziki Zuchu na mwanadada Rita Norbeth ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond Platnumz.

Hii ni baada ya video ya Zuchu kusambaa kwenye mitandao ya kijamii akiimba huku mistari ya wimbo ikiwa hivi, "Unagombana na mimi kwani ndio nilikunyima kodi?"

Mistari hiyo inatazamwa kama dongo alilotupiwa Rita kutokana na kauli aliyowahi kusema akidai Diamond alishindwa kumlipia kodi wakati wapo wenye mahusiano.

Wimbo na mistari ya Zuchu inanikumbusha mambo ya kimwambao yaliyokuwa yakifanywa na wasanii wa taarab enzi hizo. Kutupiana maneno kwa kutumia nyimbo kati ya wake wenza. Yaani ni kama enzi zile Jokha Kassim na Leyla Rashid.

Utakumbuka hekaheka za wawili hawa zilianza baada ya kuvuja kwa video zikimuonyesha Rita akiwa na nyota wa muziki, Diamond Platinumz, kwenye mahaba mazito.

Hata hivyo baada ya kuvuja kwa video hizo, Diamond akaibuka na 'kuzikana' akisema yeye na mrembo huyo walishaachana tangu mwaka 2023. Lakini bibie Rita Norbeth akaibuka na kusema anachosema Diamond si kweli. Kwani 2023 haukuwa wa kuachana, bali kubainika kwa mahusiano yao kwa Zuchu, lakini waliendelea kuwa wapenzi hadi 2024.

Rita hakuishia hapo, akaenda mbali na kulalamika kwamba alinyanyaswa kihisia na Diamond walipokuwa Afrika Kusini. Akasema Diamond alilala na mwanamke mwingine wa kuitwa Fantana, kwenye chumba kingine akimuacha yeye peke yake kwa kuwa alikuwa hedhi. 

Hata hivyo baada ya tukio hilo, Rita ameshindwa kuvumilia na kujibu kwa kudai kuwa kodi tayari imelipwa.