Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Video ya wimbo 'Jeene Laga Hoon' ilivyobadili maisha ya Krish

Muktasari:

  • Hilo limejidhihirisha kwa mtoto Krish Mondal kutoka India, mwenye umri wa miaka 9. Ambaye kupitia kipaji chake cha kuimba amefanikiwa kubadilisha maisha ya familia yake.

India. Mitandao ya kijamii inaendelea kuthibitika kuwa jukwaa lenye nguvu ya kubadilisha maisha ya watu duniani. Likiwezesha vipaji vilivyokuwa vimefichika kujitokeza na kutambulika katika pande zote za dunia.

Hilo limejidhihirisha kwa mtoto Krish Mondal kutoka India, mwenye umri wa miaka 9. Ambaye kupitia kipaji chake cha kuimba amefanikiwa kubadilisha maisha ya familia yake.

Krish, akiwa pamoja na kaka yake Kishore Mondal, walianza kutengeneza maudhui ya kuimba kwa lengo la kujifurahisha. Lakini miezi michache baadaye maudhui hayo yalianza kuwapa matumaini ya kutoboa kimaisha. Baada ya kurekodi video fupi wakiimba wimbo “Jeene Laga Hoon” wa Atif Aslam, hatua iliyowafungulia milango zaidi.

Video hiyo ilisambaa kwa kasi katika mitandao mbalimbali na kuwafikia watazamaji wengi duniani. Ambao waliwapongeza kwa uwezo wao wa uimbaji na sauti zao zilizogusa hisia za wengi. Umaarufu wao uliendelea kukua na kufikisha zaidi ya wafuasi milioni 4.5 katika ukurasa wao wa Instagram.

Kwa kuongezeka kwa umaarufu huo, maisha ya familia yao yalianza kubadilika taratibu, huku wakipata fursa za kufanya matangazo. Kutumbuiza katika majukwaa makubwa lakini pia kufanya kolabo na wasanii wengine.

Inaelezwa kuwa maisha yao yalibadilika kwa kiasi kikubwa kwani wamefanikiwa kununua nyumba mpya. Kuishi maisha yenye hadhi kidogo pia kumuhamishia Krish kwenye shule bora.

Krish Mondal alizaliwa Novemba 20, 2017 huko Howrah katika jimbo la West Bengal, India. Amekua akifanya vizuri katika mtandao wa YouTube akikusanya zaidi ya wafuasi 2.65 milioni pamoja na kutazamwa zaidi ya milioni 15 katika baadhi ya video zake.