Tuzo za Oscar 2025 hatihati

Muktasari:
- Tuzo za Oscar zilianzishwa mwaka 1929 huko Marekani zikiwa ni maalum kwa tasnia ya filamu.
Dar es Salaam. Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 96, tuzo za filamu za Oscar zinaweza zisifanyike mwaka huu kutokana na janga la moto lililolikumba jimbo la Los Angelesna vitongoji vyake hivi karibuni.
Kamati inayosimamia tuzo hizo, inaripotiwa kuwa inafanya tathmini kwa sasa kuona uwezekano wa kutofanya tukio hilo Machi 3 kama ilivyopangwa awali.
Waandaaji wa tuzo hizo wanahisi kwamba kitendo cha kuzifanya mwaka huu kitawapa taswira mbaya ya kuonekana ni watu ambao hawajaguswa na janga la moto ambalo limesababisha makumi ya watu kufariki na mamia kubaki hawana makazi.
“Wasiwasi mkubwa wa bodi ni kutoonekana kama wanasherehekea huku wakazi wengi wa Los Angeles wakipambana na mpasuko wa moyo na upotevu usiotarajiwa.
“Na hata kama moto utaisha wiki ijayo, uhalisia ni kwamba jiji linaendelea kuumia na litaendelea na maumivu hayo kwa miezi kadhaa.
“Hivyo utawala umeamua kwamba mkazo uwe kusapoti na kufanya harambee pindi fursa sahihi itakapojitokeza yenyewe,” kilifichua chanzo cha ndani.
Watu 25 wanatajwa kupoteza maisha kutokana na moto huo na namba hiyo inategemewa kuongezeka kwa vile huduma za dharura zipo katika tukio.
Zaidi ya watu 200,000 wamelazimika kuyaacha makazi yao na watu 88,000 wapo katika uokoaji.
Watu wanne wanaounda bodi ya kuandaa tuzo za Oscar ni Tom Hanks, Emma Stone, Merly Streep na Steven na Spielbeg.