Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtengeneza maudhui aliyejikondesha ashangaza wengi

Muktasari:

  • Mbali na hilo amesema video za maudhui ambayo yalikuwa yakiendelea kuonekana kwenye chaneli yake Youtube zikimuonesha akiwa na uzito mkubwa  zilirekodiwa siku za nyuma hivyo hakuna kazi mpya aliyotengeneza ndani ya miaka miwili.

Marekani, Mtengeneza maudhui wa Marekani Nicholas Perry, ‘Nikocado Avocado’, ambaye amejizolea umaarufu kutokana na maudhui yake yanayohusu chakula kwenye mtandao wa YouTube, amewashangaza wengi kutokana na mabadiliko yake ya mwili yanayoonesha akiwa amepungua uzito kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza katika video aliyoipa jina la "Two Steps Ahead” amesema amepunguza zaidi ya kilo 113 ndani ya miaka miwili.

Mbali na hilo amesema video za maudhui ambayo yalikuwa yakiendelea kuonekana kwenye chaneli yake Youtube zikimuonesha akiwa na uzito mkubwa  zilirekodiwa siku za nyuma hivyo hakuna kazi mpya aliyotengeneza ndani ya miaka miwili.

Hadi sasa video inayomuonesha Perry akiwa amepungua uzito imepata zaidi ya watazamaji milioni 30  huku komenti  zikiwa zaidi ya laki mbili kwenye mtandao wa YouTube

Hata hivyo kupitia komenti nyingi za mashabiki wameonekana kutoamini na wengine kushangaa kutokana na upunguaji huo.

"Hii nahisi kama si ya kweli ameweza kutuchezea kama kinanda, "ameandika shabiki

"Kweli aliweza kuweka siri , bila mtu yeyote duniani kujua , ni jambo gumu hata kulielewa," ameandika shabiki