Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Masheikh watoa angalizo maudhui ya vichekesho wakati wa Ramadhan

Muktasari:

  • Katika kipindi hiki cha mfungo ambacho huongozwa na swala na toba. Baadhi ya masheikh wamezungumzia wasanii kukitumia kwa kutoa maudhui ya vichekesho wakisema ni sawa na kwenda kinyume na maadili ya mwezi huu

Dar es Salaam. Wakati baadhi ya wasanii wa vichekesho wakitoa maudhui mbalimbali yanayohusu Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, wanazuoni wa dini hiyo wametoa angalizo la ujumbe na maadili katika kazi hizo za sanaa.

Katika kipindi hiki cha mfungo ambacho huongozwa na swala na toba. Baadhi ya masheikh wamezungumzia wasanii kukitumia kwa kutoa maudhui ya vichekesho wakisema ni sawa na kwenda kinyume na maadili ya mwezi huu.  

Akizungumza na Mwananchi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Amani na Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum amesema Ramadhan siyo kwa ajili ya michezo na mambo yote ya kipuuzi.

"Jambo lolote la kupumbaza ambalo lipo nje ya imani na ibada ya mwenyezi Mungu. Mwezi wa Ramadhan siyo mahali pake. Muumini wa kiislamu asipoteze hata dakika moja kufanya upuuzi, hiyo dakika aitumie kumtaja Mungu kwa sababu matendo yanayofanywa mwenzi wa Ramadhan yanalipwa mara dufu. 

"Wanaofanya komedi au vichekesho mwezi wa Ramadhan ni wale ambao hawajajua yaliyomo ndani ya mwezi huu. Miezi 11 umefanya komedi Mungu kwa fadhili zake anakupa mwezi mmoja tu wa kukusamehe yale uliyofanya miezi 11, alafu bado unakuwa siyo mwelewa,"amesema

Kwa upande wake sheikh Hamis Mataka amesema kama maudhui ya vichekesho yanania njema kwa ajili ya kifundisha hilo halina matatizo.

"Kama dhamira ni njema inakusudia kufundisha uwepo wa vitendo hivyo vya kwenye jamii mimi sioni matatizo yake. Lakini kama dhamira ni kuleta kebehi hiyo haifai," amesema

Naye sheikh Omary Billal ameiambia mwananchi kuwa ni vyema wasanii wa vichekesho wakajiepusha kutengeneza maudhui ya namna hiyo ili wajiweke sehemu salama zaidi.

"Kwa ujibu wa imani haipo sawa. Ikiwa mafundisho ambayo yanaelekeza namna swaumu inatakiwa iwe au kuwalea watoto katika ufungaji hiyo inaweza ikafaa, lakini kufanya vichekesho kutengeneza maudhui tu ili watu wacheke hapana hilo halifai,"amesema 

Mbali na viongozi hao wa dini, mchekeshaji Shafii Brand ameiamba Mwananchi baadhi ya wasanii wanaotaka umaarufu wa harakaharaka ni changamoto. Kwani wanatumia maudhui hayo kwa njia ya kupotosha.

"Waandaaji maudhui tupo wengi kila mmoja na namna yake. Dunia sasa hivi imebadilika kwanza haihitaji watu wawe 'serious' sana. Na haihitaji mtu akosee, kwa sisi ambao tumepata bahati ya vitu vyetu kuonekana kwa watu wengi. Tunaepuka hiyo kutokebei au kudharau dini.

"Mimi maudhui yangu mwisho yanafundisha. Siyo kwa sababu watu wamefunga basi tuwe 'serious' hapana wanatakiwa kupata burudani na maisha mengine yanaendelea. Kuna baadhi ya madogo ambao bado hawajapata nafasi wao wanafanya ili waweze kupata nafasi unakuta wanakiuka misingi na taratibu,"amesema Shafii

Aidha mchekeshaji Hassan Kazoa 'Chauroho' ambaye ni miongoni mwa wanaofanya maudhui yanayoendana na mwezi wa mfungo amesema ni vyema wachekeshaji kuonesha kazi zao kwa viongozi wa dini kabla hawajazitoa

"Mimi nimepitia madrasa dini naifahamu, nafanya vile kurekebisha watu ambao wana tabia kama zile waache ndiyo maana kuna makatazo ndani yake haiendi moja kwa moja kwenye kupotosha.

"Mimi hata kwa wanaoandaa maudhui yasiyo na mwisho mwema nadhani wanatakiwa wafunzwe inawezekana wakawa hawajapitia kwenye maadili ya dini. Hata mimi filamu yangu kabla sijairusha niliwatumia mashekhe waliona na wakasema ipo sawa,"amesema wakati akizungumza na Mwananchi