Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chege hana mpango wa kifanya biashara kwa sasa

Muktasari:

Msanii kutoka kundi la TMK Wanaume Family Chegge Chigunda amesema kuwa hivi sasa hafanyi biashara yeyote tena ameamua kujishughulisha na muziki tu.

Msanii kutoka kundi la TMK Wanaume Family Chegge Chigunda amesema kuwa hivi sasa hafanyi biashara yeyote tena ameamua kujishughulisha na muziki tu.

Awali msanii huyo alikuwa alifungua duka la nguo ambalo lilikuwa likiuza nguo za wanaume na wasichana maeneo ya Kinondoni, baadae msanii huyo pia alikuja kufungua saloon ya kiume lakini nayo haikukaa kwa muda mrefu ikafungwa.

Chegge alisema kuwa sababu za kuamua kutokufanya biashara tena nikutokana na ugumu aliopata kusimamia biashara hizo hivyo kumpa hasara,

"Biashara inaumiza kichwa sana, mtu unawezeka pesa yako lakini ukija kupiga mahesabu unakuta ni hasara tu ndo maana nimeamua hivi sasa niachane nazo kwa kuwa muda mwingi anautumia kufanya shughuli za sanaa.

Msanii huyo anasema kuwa kwa sasa anajishughulisha na muziki peke yake, na pia filamu za kwake na si za watu.

Alitoa mfano wa filamu ambayo anaiandaa hivi sasa ni filamu ya wimbo wa 'Mwanayumba' ambayo stori yake itatokana na wimbo huo.Chegge pia alisema kuwa video ya wimbo wake alioutoa mwaka huu 'Uswazo Take Away' tayari imetoka.

Video ilitengenezwa chini ya muongozaji maarufu hapa Tanzania Adam Juma wa kampuni ya Visual Lab. Na pia kuna wasanii na watu maarufu ambao wako katika video hiyo kama Jackin Wolper wa bongomovies, Bi Cheka na msanii kutoka Tip Top Madee.