Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zanzibar yazindua muongozo lishe shuleni kuongeza ufaulu

Unguja. Ili kuwasidia wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu na kuongeza ufaulu wao, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imezindua muongozo maalumu wa ulishaji chakula mashuleni visiwani humo.

Muongozo huo ambao umeandaliwa kwa usimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), unalenga kuwasaidia wanafunzi wa shule zinazokabiliwa na mazingira magumu ili kuinua ufaulu.

Katika hotuba iliyosomwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar leo Novemba 14, 2023, Ali Abdugulam Hussein kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Suleiman Abdulla amesema kwamba imani yao wadau wataufuata muongozo huo ili kuepusha na matokeo hasi ya chakula kisichozingatia mahitaji halisi ya watoto.

“Pamoja na umuhimu wa miradi ya ulishaji wa chakula katika shule zetu, bado kulikuwa na upungufu wa miongozo ya ulishaji wa chakula, ambapo wadau walitumia fursa hiyo kuwalisha watoto bila kufuata miongozo,” alisema

Amesema mwaka 2014 ulianzishwa mradi wa “Home Grown School Feeding” kwa kipindi cha majaribio katika Wilaya mbili za Kaskazini A Unguja na Micheweni Pemba, ambapo shule tisa zilijuimwa, na baadaye mpango huo ulizifikia shule 36 na kwamba shule nyingine sita zikitarajiwa kuongezwa.

“Jumla ya wanafunzi wanaonufaika na mradi huu mpaka kufikia Septemba mwaka huu ni 20,807 na malengo ni kufikia shule 50 ifikapo mwaka 2025,” amesema

Mkurugenzi Mkazi wa WFP, Sarah Gibson amesema wataendelea kuisaidia serikali katika mipango yake mbalimbali ili kuinua uchumi wa mwananchi mmojammoja na taifa kwa ujumla.

Sarah amesema mpango huo wa lishe ni muhimu kwani utasaidia watoto kupata lishe bora na kuinua viwango vya ufaulu.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Khamis Abdallah Said amesema hakuna mtoto asiyekuwa na akili bali inatokana na changamoto wanazopitia ikiwemo tatizo la lishe na jinsi wanavyoandaliwa.

Amewataka wazazi na jamii kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha masuala ya lishe yanahimizwa ili kuwasaidia wanafunzi kupata elimu bora.

Naye mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Fujoni, Mkubwa Hamad Hassan amesema mtoto anapokuwa na lishe bora hata shuleni anabaki darasani na anakuwa na usikivu mzuri kutoka kwa mwalimu.

Mkurugenzi Idara ya Maandalizi na Msingi, Fatma Ramadhan amesema mpango huo pia utasaidia kupunguza utapiamlo na wanafunzi wengi watapata fursa ya kusoma kwa kubaki shuleni kipindi chote cha masomo.