Mbaroni akidaiwa kumchoma kisu mke mwenza

Muktasari:
- Tukio hilo limetokea baada ya mke mkubwa aliyekuwa na kisu kumshambulia mke mdogo alipokuwa akishuka kwenye gari akiwa na mume wao.
Unguja. Maimuna Suleiman Said (38) mkazi wa Chukwani amejeruhiwa kwa kukatwa na kisu mwilini na mke mwenza kwa madai ya wivu.
Akizungumza leo Februari 12, 2025 kuhusu tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa Mjini Magharibi, Richard Mchonvu amesema tukio hilo lilitokea Februari 9, 2025 saa saba mchana huko Chukwani, ambapo Khadija Ali Shaaban (34) ambaye ni mke mwenza anadaiwa kutenda kosa kwa wivu wa mapenzi.
“Hawa ni mtu na mke mwenza, mke mkubwa ndio alimkatakata visu mke mdogo, wote watatu na mumewe wao walikuwa kwenye gari walipofika nyumbani kwa mke mdogo wakashuka, lakini hakuna aliyejua kama mke mkubwa ana kisu akamshambulia mwenzake,” amedai.
Kwa mujibu wa Mchonvu, baada ya kushambuliwa mwanamke mdogo alipiga kelele na yule mwanaume akatoa msaada kisha kumpeleka majeruhi katika hospitali ya Lumumba na mtuhumiwa alipelekwa Kituo cha Polisi Mazizini.
“Mpaka sasa tunamshikilia hatua zigine zinaendelea ili kumfikisha mahakamani kwa sbabu lilikuwa ni tukio la wazi,” amedai Mchonvu.
Naye Khadija aliyejereuhiwa amedai alikuwa katika matembezi na mume wake (hakutajwa jina) baada ya kumailiza kikao wakarudi kwenye gari kumbe alikuwa amewasiliana na mke mkubwa na walimpitia wakampakia kueleka nyumbani.
“Mimi ndio nilikuwa naendesha gari tulipofika njiani kumbe mume wangu alikuwa anawasiliana na mke wake, tukampakia na kwenda naye nyumbani, lakini tulipofika alikataa kushuka.
“Mimi nilishuka baada ya kumpa mgongo kumbe alikuwa na kisu akaanza kunikata mgongoni nilipogeuka akanikata usoni nikaanza kupiga kelele kuomba msaada,” amedai.