Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bei za petroli, dizeli zapaa Zanzibar

Meneja wa Kitengo cha Uhusiano Zura, Mbaraka Hassan Haji akitangaza mabadiliko ya bei mafuta Zanzibar. Picha na Zuleikha Fatawi

Muktasari:

  • Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (Zura) inapanga bei za mafuta kwa kuzingatia mambo mbalimbali, ikiwemo mwenendo wa bei za mafuta duniani, gharama za uingizaji wa mafuta Bandari ya Tanga, mabadiliko ya fedha za kigeni, gharama za usafiri, bima, kodi za Serikali, na faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja.

Unguja. Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (Zura) imetangaza kuongezeka kwa bei za mafuta ambazo zitaanza kutumika leo Jumatano, Aprili 9, 2025.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo, Meneja wa Kitengo cha Uhusiano wa Zura, Mbaraka Hassan Haji, amesema kuwa ongezeko hilo la bei linachangiwa na mabadiliko ya fedha za kigeni dhidi ya Shilingi ya Tanzania.

Amesema kwa Aprili, bei ya petroli itakuwa Sh2,949 kwa lita kutoka Sh2,939 ya mwezi uliopita, ikiwa ni ongezeko la Sh10, sawa na asilimia 0.34.

Mafuta ya dizeli lita moja itauzwa kwa Sh3,194 kutoka Sh3,135, tofauti ya Sh59, sawa na asilimia 1.88, na mafuta ya ndege yatauzwa Sh2,537 kwa lita kutoka Sh2,500, sawa na ongezeko la Sh37, ikiwa ni asilimia 1.48.

"Bei ya mafuta ya taa yataendelea kuuzwa kwa bei ile ile ya Sh3,200," amesema.

Hata hivyo, meneja huyo amesema ZURA inapanga bei kwa kuzingatia mambo mbalimbali, ikiwemo wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta duniani, gharama za uingizaji wa mafuta katika Bandari ya Tanga.

"Pia, Zura inaangalia gharama za mabadiliko ya fedha za kigeni zinazotumika kununulia mafuta, gharama za usafiri, bima na ‘Preminium’ hadi Zanzibar, kodi za tozo za Serikali na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja," amesema Mbaraka.

Amesisitiza kuwa bei za mafuta kwa mwezi huu zimeongezeka kutokana na mabadiliko ya Fedha za kigeni kwa Shilingi ya Tanzania.

Sambamba na hayo, mamlaka hiyo inawahimiza wananchi kununua mafuta katika vituo halali vya kuuzia mafuta na kudai risiti za kieletroniki kila wanaponunua mafuta hayo ili zinapotokezea changamoto zozote wapate kusaidiwa.

Huba Juma ametoa maoni kuhusu ongezeko hilo la bei za  mafuta amesema Serikali inasisitiza kuwa gharama za nishati hizo zitapungua bei, ila kila siku zinavyosogea ndivyo nishati hiyo inavyozidi kupanda bei.

Ameeleza kuwa Serikali inapaswa kutambua kuwa waathirika wa bei hizo ni wananchi, hivyo wanatakiwa kuangalia upya mwenendo wa bei hizo.