Smart Gin inaunga mkono juhudi za kukuza uchumi kupitia ulipaji kodi

Kinywaji cha Smart Gin.

Kodi ni msingi wa maendeleo ya Taifa kwa sababu ndizo zinazotumika katika kutengeneza ustawi wa Taifa kwa kuboresha huduma za jamii na miundombinu.

Kodi hizi hulipwa kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo ajira, kampuni, mashirika, taa¬sisi wajasiriamali na wafanya¬biashara ambao kwa jina moja wote hutambulika kama walipa kodi.

Walipa kodi ni kundi muhimu katika ukuaji wa uchumi na maendeleo kwa sababu kodi ndizo zinaiwezesha Serikali kutekeleza mambo mbalimbali ya kimaendeleo.

Kwa kutambua umuhimu wa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitan¬gaza Novemba kuwa mwezi maalumu kwa ajili ya kutoa shukrani kwao.

Pamoja na mambo mengine mamlaka hiyo ililenga kurudi¬sha shukrani kwa walipa kodi na wadau wa kodi wote nchini kwa juhudi na mchango wao katika maendeleo ya Taifa.

Miongoni mwa mambo ambayo TRA wanayafanya ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho hayo ni kuandaa mbio na matembezi ya shukrani kwa mlipakodi pamoja na tuzo ambazo wanazitoa kwa wali¬pa kodi bora katika makundi tofauti.

Moja ya washindi katika tuzo hizo ni kampuni ya Euromax Limited ambayo ilishinda tuzo ya mlipa kodi bora mkoa wa kikodi wa Ilala katika kipengele cha walipa kodi wakubwa.

Kampuni ya Euromax Lim¬ited ambayo ni mzalishaji na msambazaji wa kinywaji cha Smart Gin imetambuliwa kwa mchango wake muhimu katika suala la ulipaji kodi. Tuzo hiyo inathibitisha jukumu lao la kuwekeza kwa uwazi na kufuata sheria za kodi.

Tuzo ya mlipa kodi bora Mkoa wa kikodi wa Ilala katika kipengele cha walipa kodi wakubwa ambayo kampuni ya Euromax Limited imeshinda.

Kampuni hiyo inaonyesha mfano wa kuigwa katika sekta ya uzalishaji viwandani na ina¬leta imani kwa wadau kwa kuon¬yesha utayari wao wa kuchan¬gia maendeleo ya jamii kupitia ulipaji kodi.

Baada ya kupata tuzo hiyo gazeti hili lilipata nafasi ya kufanya mahojiano na Mku¬rugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Peter Michael Kinabo ambaye alieleza mafani¬kio nyuma ya tuzo hiyo.


Hongereni kwa kupata tuzo ya mlipa kodi bora. Tuzo hii ina maana gani kwenu?

Kwanza tunawashukuru wateja na washirika wetu kwa kutuamini, tunawaambia kwamba tunathamini imani yao kwetu na tunawahakiki¬shia tutailinda kwa kuendelea kuwapa bidhaa bora.

Tunaishukuru TRA kututambua kwamba tunafuata taratibu za kodi. Hii imetupa moyo na hamasa ya kuendelea kufua¬ta sheria za kodi nchini kwa sababu sisi tunafanya kazi na wadau mbalimbali ambao wanazingatia kufuata tara¬tibu, sheria na kanuni zote ikiwemo za kodi.

Hivyo tuzo hii imetuon¬gezea kuaminika kwa washiri¬ka wetu lakini pia Serikali na wateja wetu kwa sababu ime¬onyesha ni namna gani tunatii sheria zilizowekwa na mam¬laka husika.

Tuzo hii pia ni ishara ya kufanya kazi kwa kuzinga¬tia weledi na kuweka juhudi, kusimamia ubora na uhusia¬no mzuri na taasisi nyingine. Tunajivunia kuwa sehemu ya kuisadia Serikali kutekeleza mipango mbalimbali ya kimaendeleo na kutoa huduma bora kwa wananchi.


Ni ipi nafasi ya mkurugenzi katika mafanikio haya?

Eoromax Limited ni kati ya kampuni bora nchini zenye uhusiano mzuri kati ya mwajiri na wafanyakazi. Wafanyakazi wanahusika kikamilifu kwenye mipango mikakati ya kampuni kuanzia ngazi ya chini ya utend¬aji hadi ya juu ya maamuzi.

Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi wa tuzo za walipa kodi bora kwa mwaka 2022/2023 wakati wa hafla ya ugawaji wa tuzo hizo iliyofanyika Desemba 1, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kupitia Mkurugenzi Mtend¬aji Mkuu, kampuni ya Eoromax Limited imefanikiwa kuibuka kinara katika kipengele cha walipa kodi wakubwa Mkoa wa kikodi wa Ilala.

Kupitia juhudi zake katika kuhamasisha na kuwa mfano bora kwa wafanyakazi, kampuni hii imeweza kupata mafanikio makubwa ya kiutendaji ikiwe¬mo tuzo hii. Siku zote ame¬kuwa akisisitiza kuwa bidhaa tunazozitoa ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya Watanza¬nia pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

Amekuwa akihimiza uwa¬jibikaji na ushirikiano katika kampuni kwa kufanya kazi kwa bidii, kujituma na kuweka dira na dhamira ya kampuni mbele.


Hii ni mara ya ngapi Euromax Limited kupata tuzo hii?

Hii ni mara ya pili kushinda tuzo hii ambapo mwaka uliopita tulifanikiwa kushika nafasi ya tatu katika kipengele cha walipa kodi wakubwa Mkoa wa kikodi wa Ilala.


Kwa kiasi gani tuzo hii itaonge¬za hamasa katika kuendelea kutoa bidhaa bora na kulipa kodi?

Tuzo hii ni kama deni kwetu sisi katika kuhudumia wateja wetu kwa kuwa bado tuna deni kubwa kwao la kuhakikisha tunaendelea kuboresha bidhaa zetu ili ziendane na mahitaji yao ya kila siku.

Pia imetupa hamasa ya kuen¬delea kufuata sheria na kanuni za kodi kwani tunaamini kulipa kodi ndiyo msingi wa maende¬leo ya kweli kwa sababu kodi hizo ndizo zinawezesha Serikali kutoa huduma kwa wananchi na kutekeleza mikakati ya maendeleo.


Ni uzoefu gani mmeupata kwa kushiriki tuzo hizi?

Kikubwa ni kukutana na mashirika na taasisi zinazofan¬ya biashara nchini, kukaa meza moja na kubadilishana uzoefu ni jambo kubwa ambalo tume¬lipata kwa kushiriki tuzo hizi.


Mikakati yenu ni ipi katika kue¬ndelea kufanya vizuri kwe-nye tuzo hizi mwakani?

Mkakati mkubwa ni kuende¬lea kuboresha mifumo yetu ya ndani ili kuhakikisha inaendelea kuwa bora jambo litakalorahi¬sisha utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kikodi na hivyo kutufanya kuendelea tulipoishia mwaka huu.

Kingine ni kuendelea kubore¬sha utoaji wa bidhaa kwa wateja wetu. Tutahakikisha tulichofan¬ya mwaka huu tunakifanya mara mbili au tatu hapo mwakani hivyo wateja na washirika wetu wakae mkao wa kula mambo mazuri yanakuja.