Miaka 20 ya jasho, mafanikio katika sekta ya vilipuzi ya Nitro Explosives Ltd


Baada ya miaka mingi ya uchapakazi, kujitoa na uvumbuzi, Kampuni ya Nitro Explosives, ambayo bado haifahamiki na Watanzania wengi, sasa inatimiza miaka 20.

Kampuni hiyo inajihusisha na vilipuzi salama vya kibiashara vinavyotumika katika uchimbaji madini na miradi ya miundombinu.

Ilianzishwa mwaka 2002 ikiwa ni matokeo ya uwekezaji wa wakurugenzi na wanahisa wa Nitro.

Wazo la biashara hiyo lilianzia kwa mmoja wa waanzilishi wa kampuni hiyo, Bw. Johan Viljoen kuamua kufanya kitu sahihi katika sekta ya uchimbaji mdogo wa madini.

Alishirikiana na mfanyabiashara wa Kitanzania na hatimaye tarehe 22 – 02 – 2002, shehena ya kwanza ya vilipuzi vya kibiashara ilifika baada ya mchakato wa muda mrefu wa kupata leseni ya kufanya biashara.

Kampuni ilianzia chini kabisa mpaka kufikia kuwa kiongozi wa soko—milima na mabonde waliyoyapitia katika kuisimamisha kampuni hiyo yanatosha kuwekwa katika vitabu.

Nitro, pamoja na mwelekeo wake wa ukuaji, imejitofautisha na wengine kwa kuwa kampuni bora zaidi na sio kubwa zaidi.

Johan amezungumza na Mwananchi kuhusu mambo machache kuhusu shughuli za kampuni kuelekea katika maadhimisho ya miaka 20 ya kampuni hiyo.

Swali: Watanzania hawaifahamu kampuni ya Nitro Explosives vyema. Tuelezee kwa ufupi kuhusiana na kampuni hiyo.

Kampuni ya Nitro inabebwa na watu wake, na mimi ninawachukulia wafanyakazi wangu kama familia na siyo waajiriwa. Wafanyakazi wana tabia ya kuwahudumia wateja na watu wengine kwa ujumla kwa unyenyekevu.

Pia Nitro ni Pamoja na kuwa na wateja wake waaminifu. Mara zote tumekuwa tukiwapa kipaumbele wateja wetu na kuwasaidia pale wanapohitaji msaada wa kiufundi na bidhaa bora.

Nitro inaongozwa na ushirikiano wenye nguvu. Mwaka 2017 kampuni ya kimataifa ya Austin Powder Africa Inc. kutoka Marekani ilinunua hisa za Nitro na kuwa mwanahisa.

Pia shukrani zangu zimfikie mke wangu na wanangu kwa uelewa wao na uvumilivu.

Swali: Shughuli kuu zinazofanywa na Nitro ni zipi?

Uhifadhi na usambazaji salama wa vilipuzi vya kibiashara kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Hii hufanyika kuanzia kwenye miradi ya miundombinu, migodi ya kati hadi ile midogo. Barabara nyingi tunazotumia leo zilitengenezwa baada ya Nitro kufanya ulipuaji katika maeneo hayo.

Kwa sasa, Nitro ndiyo kampuni pekee ya ulipuaji inayoshiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) nchini katika michorongo, migodi ya kokoto, na kutoboa mahandaki.


Hivi karibuni, tumeanza kutengeneza vilipuzi vya emalshani kwa majaribio hapa nchini kwa kutumia teknolojia ya Marekani na hii itakapokamilika tunaweza kuiita bidhaa halisi ya Kitanzania.

Tunatarajia kuzalisha bidhaa zaidi ndani ya nchi licha ya kuwa malighafi zote huagizwa kutoka nje katika tasnia hii.

Swali: Kampuni inaadhimisha miaka 20 ya biashara yake ya vilipuzi salama nchini. Hii ina maana gani?

Jibu lake ni rahisi tu, pongezi kwa kila mtu katika kampuni ambaye alifanya kazi kwa bidii na kuwa mwaminifu kwa kampuni.

Swali: Je, unaonaje mwenendo wa soko la sekta ya vilipuzi nchini? Je, inakua au imebaki pale pale?

Kwa sekta ya vilipuzi vya kibiashara, inakua kwa kampuni za vilipuzi zinazozingatia maadili ya kiwango cha juu ya sekta hii. Hii ina maana uendelevu.

Sekta ya uchimbaji madini yenyewe inakua kwa sababu madini yako hapa nchini na mahitaji ya kuuza nje ya nchi na uchakataji yapo. Na Kwa idadi ya watu inavyoongezeka kwa kasi, hakuna njia nyingine.

Nitoe rai kwa Wadhibiti ya kwamba wanapaswa kufanya maamuzi mazuri yenye manufaa kwa Tanzania na watu wake. Sekta haitakuwa kama kutakuwa na upindishaji wa kanuni au taratibu.

Pia wadau katika sekta hii wanapaswa kuanza kujikita katika matumizi ya teknolojia mpya na bidhaa bora za kuaminika. Dhana ya unafuu mara nyingi huwa ni ghali Zaidi ya inavyodhaniwa.

Swali: Je, mambo gani ambayo hatufahamu kuhusu vilipuzi?

Watu wanaofanya kazi katika sekta ya vilipuzi si wengi. Hivi ndivyo inavyopaswa kuwa.

Ikiwa mtu yeyote ataona gari lililo na bendera nyekundu na maandishi "milipuko" au "baruti" au ishara ya rangi njano ya vilipuzi au "mzigo wa hatari" unatakiwa kukaa kando, ukae umbali salama.

Ikiwa gari la vilipuzi kwa mfano limehusika katika aina fulani ya ajali - kimbia, kaa mbali, mbali zaidi.

Swali: Je, kampuni hii inachangiaje katika ukuaji wa uchumi wa nchi?

Tunatoa fursa za ajira kwa kadri tunavyoendelea kukua na kulipa kodi. Pia, jitihada zetu za kujaribu na kuwanyanyua wachimbaji wadogo ili kuwawezesha kukua kufikia katika biashara za kati au kubwa.

Natumai kwamba wachimbaji wadogo wanaweza kuelewa na kuwekeza zaidi katika migodi yao na kuachana na mawazo ya kuanzisha miradi mingine.

Swali: Je, ni nini kinapaswa kurekebishwa na Serikali ili kusaidia kuendeleza sekta hiyo ndogo?

Serikali haitapunguza mzigo wa kodi. Kwa hivyo, ikiwa idara za Serikali zinaweza kuwasiliana zenyewe kwa zenyewe na kuweka sawa mazingira ya ufanyaji biashara, itakuwa chachu ya ukuaji endelevu wa sekta.

Swali: Kampuni inatamani kuwa wapi baada ya miaka mitano hadi kumi kuanzia sasa?

Kuna mpango wa ukuaji au maendeleo. Lengo la kwanza la kampuni ni kutanua wigo wake nchini, kuzalisha bidhaa nyingi zaidi ndani ya nchi na kisha kuuza zaidi kwa nchi za jirani.

Tanzania inaweza kuwa nchi kinara kwa kuwa ndiyo yenye uzoefu mkubwa wa uchimbaji madini Afrika Mashariki, sambamba na bandari na mtandao mzuri wa barabara.

Nahitimisha kwa kusema kuwa, dhana ya bidhaa za bei nafuu ni ghali zaidi kutokana na bidhaa hizo kutokufanya kazi kwa usalama na kwa kiwango cha chini.

Mawasiliano Zaidi ya Nitro Explosives Ltd ni kama ifuatavyo:

Barua pepe: [email protected]

Simu za kitengo cha mawasiliano: +255 684 700004; 0272 548 576