Mazingira bora kwa wafanyakazi yaibeba East-West Seed tuzo za mwajiri bora

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof Joyce Ndalichako (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo ya mwajiri wa mwaka 2023.

Tuzo ni njia muhimu ya kutambua na kuthamini mafan¬ikio katika maeneo mbalimbali ya maisha yetu. Inaweza kuwa ni kwenye sanaa, michezo, sayansi, au hata maendeleo ya kijamii. Tuzo hutoa motisha kwa watu kufanya kazi kwa bidii na kufikia malengo yao, huku ikiimarisha ubora na ubunifu.

Taasisi ama watu wanapopokea tuzo hujisikia kuthaminiwa na kutambuliwa kwa mchango wao, hivyo kujenga hisia za kujiamini na kujitambua. Hii inaweza ina athari kubwa kwa maendeleo binafsi na kitaaluma.

Kwa jamii, tuzo hutoa mifano chanya na kuhamasisha vijana na wadau wengine kufuatilia ndoto zao. Pia, huchochea ushindani chanya, kukuza ubunifu katika maeneo mbalimbali. Taasisi inapojitahidi kufikia viwango vya tuzo, wanaweza kuleta mabadiliko chanya kwa jamii na dunia kwa ujumla.

Hata hivyo, ni muhimu kuzingatia kuwa tuzo zinapaswa kutolewa kwa msingi wa viwango vya kimataifa ili kuhakiki¬sha kuwa zinaendeleza ubinufu na uchapakazi katika jamii. Kwa njia hii, umuhimu wa tuzo unaweza kudumu na kuwa na athari chanya kwa maendeleo endelevu.

Haya ndiyo Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) huyazingatia katika utoaji wa tuzo za mwajiri bora wa mwaka. Taasisi hiyo imekuwa ikithamini mchango wa waajiri kwa kuwapatia tuzo wale wanaofanya vizuri katika kutengeneza mazingira bora na salama ya kazi kwa wafanyakazi wao.

Kampuni ya East-West Seed ni miongoni mwa taasisi ambazo zinafanya vizuri katika eneo la rasilimali watu jambo lililosababisha kushindwa tuzo ya mwajiri bora kwa kampuni ndogo katika tuzo za waajiri bora mwaka 2023.

Gazeti hili lilifanya mahojia¬no na Meneja Rasilimali Watu wa East-West Seed, Yustina Joseph Waka ambaye alieleza siri nyuma ya ushindi wa tuzo hiyo. Mahojiano hayo yalikuwa kama ifuatavyo;

Hongereni kwa kuibuka wash¬indi wa tuzo za mwajiri bora wa mwaka 2023 – Kipengele cha Taasisi Bora Ndogo. Mnajisikiaje kupokea tuzo hii?

East-West Seed tumefurahi sana, kwani hii ni tuzo kubwa kwetu na imetupa motisha chanya ya kuendeleza kujenga mazingira bora ya kazi na kutoa huduma iiyo bora wa jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited, Bakari Machumu (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya East-West Seed, Robert Kimonge kikombe cha ushindi wa mwajiri bora wa mwaka ambacho kampuni hiyo imeshinda katika kipengele cha kampuni ndogo.

Hii ni mara ya ngapi mnashiriki na kushinda tuzo hii?

Tulishawahi kushiriki mara moja hii ni mara ya pili na tumeweza kushinda tuzo hili.

Kuna taasisi nyingi zilizoshiriki katika tuzo hizo mnadhani nini kimewafanya kuwa bora zaidi ya wengine na hadi kushinda nafasi hiyo?

Ni kweli kwamba taasisi zaidi ya 91 zimeweza kushishiriki katika tuzo ya mwajiri bora mwaka huu zikiwemo za kati na ndogo pia vigezo vingi vilizingatiwa. Ushindi wetu ni kutokana na kukidhi vigezo vilivyoweka kwa asilimia 100.

East-West Seed tumezipa kipaumbele nyanja tofauti tofauti katika utendaji kazi wetu ili kuhakikisha kuwa wafanyakazi wetu wanakua na mazingira bora ambayo ni pamoja na mazingira yenye tija, mawasiiano ya uaminifu, fursa za ukuaji, fikra chanya, usawa mzuri wa maisha ya kazi na ushiriki mzuri wa timu wenye tija.

Pia East West Seed imekua mstari wa mbele katika kuchan¬gia pato la Serikali kwa nam¬na tofauti ikiwemo ulipaji wa kodi, mauzo na manunuzi ya ndani. Lakini pia kuisaidia jamii inyotuzunguka ni kipaumbele kwetu.


Ushindi huu una maana gani kwa East West Seed?

Tuzo hii ina maana kub¬wa sana kwa jumuia nzima ya East-West Seed. Tuzo hii ni utambulisho mzuri wa huduma tunazotoa kwa wakulima, jinsi tunavyowajali waajiriwa wetu, tunakidhi taratibu za kiserika¬li na kuifanya East -West Seed kuwa mfano kwa waajiriwa wengine ambao hawajapata tuzo hii.

Kwa kiasi gani ushindi wenu unaakisi utendaji kazi wenu?

Ushindi huu umetupa motisha kubwa na kuwa utambulisho kwamba East-West Seed ni sehemu sahi¬hi ya kufanya kazi ambayo pia inatoa huduma bora kwa jamii ikiwemo kuwa¬hudumia wakulima wado¬go wadogo.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya East-West Seed, Robert Kimonge (kulia) akiwa na Meneja Msaidizi wa Rasilimali watu wa kampuni hiyo, Salim Mgonja wakiwa wameshika tuzo ya ushindi wa mwajiri bora wa mwaka katika kipengele cha kampuni ndogo.

Maeneo gani yamekuwa bora zaidi katika utendaji wenu?

Maeneo yaliyokua bora zaidi ni pamoja na uongo¬zi na utawala bora, ubora katika rasilimali watu, uku¬zaji na utunzaji wa vipaji, ushirikiano wa wafanyaka¬zi, usimamizi wa utendaji na utoaji wa mafunzo kwa wafanyakazi wetu.


Tuelezee kuhusu sera yenu ya ajira ilivyo

Sera yetu ya ajira inaz¬ingatia wafanyakazi wetu kama kiini cha shirika letu, hivyo huwa tunawajali katika maeneo yote ikiwe¬mo mishahara bora, afya kwa ujumla, ukuzaji, utun¬zaji na uendeezaji wa vipa¬ji, ushirikiano wa wafanya¬kazi na ajira endelevu.


Mmejipangaje kuhakikisha mnashiriki tena na kuwa wa kwanza?

Nia yetu ni kuwa mwa¬jiri bora wa mwaka hivyo tayari tumekwisha pata mrejesho wa maeneo gani ya kuboresha na kwamba tupo tayari kuwekeza kati¬ka hilo.

Lengo ni kuwa mwajiri bora kwa kukidhi vigezo vyote ambavyo ni vyanzo vya kutoa huduma bora kwa jamii na kuendelea kuwa na mazingira chanya ya kazi.

Pia tumejiwekea malen¬go yenye tija katika kuhaki¬kisha kampuni inakidhi uhitaji wa kuwa kampuni bora katika kutoa huduma zenye ubora kwa wakuli¬ma/jamii kuweka mazingi¬ra chanya ya kazi.

Hii ikiwemo kujikita zaidi katika uongozi na utawala bora, ubora katika rasilimali watu kusimamia utofauti na ushirikishwaji, ubora, tija na uvumbuzi katika shughuli zetu.


Vipi kuhusu mafanikio na changamoto?

Mpaka sasa East-West Seed ina mafanikio makub¬wa hasa katika kuwa¬hudumia wakulima wado¬go, hilo limechangiwa na kampuni kutoa kipaumbele kwenye mazingira bora ya kazi ambayo imeku¬wa motisha kubwa kwa wafanyakazi na kuwa na wafanyakazi wenye vipaji ambao wamekua kwenye kampuni kwa mda mrefu.

Licha ya mafanikio hayo, East-West Seed pia inaji¬tahidi kukabiiana na chan¬gamoto tofauti hasa katika ushindani wa kupata waa¬jiriwa wenye vipaji vya juu na pia kuhakikisha tunali¬pa mishahara yenye ushin¬dani katika soko ili kubaki na vipaji hivyo kwa mda mrefu.