CAPS Limited: Chaguo sahihi la huduma za vyoo vya kukodi, viuatilifu vya kuangamiza visumbufu

Nyumba ni choo! Huu ni usemi ambao hutumika mara nyingi ukiangazia umuhimu wa choo bora na huduma za usafi nyumbani.

Hii ni kutokana kwamba huduma hizo zina mchango mkubwa katika kujenga uchumi imara kwani ukosefu wa huduma hizo katika maeneo ya kazi na majumbani una madhara makubwa katika kupunguza uzalishaji.

Takwimu mbalimbali za Umoja wa Mataifa zimeonyesha kuwa magonjwa ya kuambukiza ikiwemo ukosefu wa vyoo na huduma za usafi zinasababisha madhara makubwa wakati mwengine mpaka vifo katika maeneo ya kazini.

Takwimu hizo pia zinaonyesha kuwa ikiwa huduma hizo zitapewa kipaumbele uchumi duniani waweza kukua kwani fedha nyingi zinapotea kila mwaka kwa kukosa huduma za vyoo, usafi na maji safi na salama.

Kutokana na jambo hilo, ndiyo maana Novemba 19 kila mwaka ni siku ya choo duniani ambapo dunia hukum¬bushwa kuwa choo na huduma za maji safi ambazo hazipewi umuhimu zinaweza kuchangia ukuaji wa uchumi. Maadhimisho ya siku ya choo duniani mwaka huu yaliongozwa na kaulimbiu ya “Kuharakisha mabadiliko”.

Kwa Tanzania siku hii huadhimishwa na Serikali na wadau mbalimbali kwa kutoa elimu kupitia njia mbalimbali kama vile vyombo vya habari, makongamano na mitandao ya kijamii kuelezea umuhimu wa huduma hizo.

CAPS Limited ni miongoni mwa wadau wakubwa wa huduma za vyoo, viuatilifu vya kuangamiza visumbufu na usafi wa mazingira ambayo imekuwa ikifanya shughuli hizo kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Peter Marealle anasema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1997 na inajihusisha na uuzaji na usambazaji wa viuatilifu vya kuangamiza visumbufu, uuzaji wa vyoo visivyotumia maji, uuzaji wa vimeng’enya (Bio-Enzymes), ukodishaji wa vyoo kwa ajili ya shughuli mbalimbali kama vile; harusi, mikutano, maeneo ya ujenzi, mazishini nk.

Anasema kampuni hiyo imekuwa ikitoa huduma kwa watu binafsi, Serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali nk.

Kuhusu wazo na sababu ya kuamua kufanya biashara hiyo, Marealle anasema “Siku moja nilikutana na jamaa mmoja kutoka Afrika Kusini aliyekuja Tanzania kuonyesha vyoo vyake katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) ambapo tulikubaliana kuanzisha uhusiano wa kibiashara. Baadaye niliamua kuanza kuuza vyoo visivyotumia maji ambavyo vilikuwa ni aina mpya nchini.”

Anasema kutokana na kuwa vyoo vile vilikuwa ni utamaduni mpya ambao haujazoeleka Tanzania akashindwa kuendelea na biashara.

“Kupitia vyoo hivyo ndipo nilipata wazo la kuanzisha huduma za vyoo vya kukodi ambavyo niliona kuna uhitaji mkubwa. Japokuwa navyo vilikuwa havijazoeleka lakini utamaduni wake ulikuwa rahisi kupokewa na Watanzania,” anasema Marealle.

Anasema huduma hiyo imesaidia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa sababu zamani ilikuwa kukiwa na shughuli ya nje watu wanakosa sehemu nzuri ya kujisaidia.

Anasema choo cha kwanza walikijenga wenyewe kwa kutumia vitu mbalimbali kama mbao na mabati na wakafani¬kiwa. Baadaye wakaendelea na biashara hiyo kwa kutu¬mia vyoo vya kutengeneza wenyewe mpaka sasa wanaa¬giza vyoo bora kutoka kwa watengenezaji wanaotambu¬lika duniani.

Anasema katika kipindi cha miaka zaidi ya 20 ya kufanya biashara hiyo wanajivunia utamaduni huo kupokelewa na Watanzania, kupunguza ucha¬fuzi wa mazingira, kuwezesha baadhi ya miradi mikubwa kuweza kutekelezeka kutoka¬na na kutoa huduma bora za vyoo pamoja na kuwahudumia Watanzania katika shughuli zao mbalimbali.

Marealle anasema wameku¬wa wakifanya juhudi mbalim¬bali katika kutoa elimu kupitia makongamano, warsha, vyom¬bo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu umuhimu wa huduma bora za vyoo ili kui¬saidia Serikali kukabiliana na changamoto ya uchafuzi wa mazingira.

Anasema kwao kipaum¬bele ni kutoa huduma kisha biashara baadaye kwa sababu wanaamini choo ni huduma ambayo kila mtu anastahili kuipata tena ikiwa katika hali ya ubora na salama.

“Ukija kwetu tunatangu¬liza kwanza huduma na ndiyo maana mtu akikodisha choo anapata na huduma nyingine kama vile dawa za kusaifishia, vitakasa mikono pamoja na mhudumu ambaye atakisi-mamia mpaka mwisho wa matumizi ya mteja,” anasema Marealle.

Anasema huduma zao hazii¬shi katika kukodisha vyoo bali pia wamekuwa wakitoa hudu¬ma za viuatilifu vya kuangam¬iza visumbufu (pest control), ukodishaji wa mahema kwa ajili ya shughuli mbalimbali, ukodishaji wa mashine za kunawia mikono, ukodishaji wa mafeni kwenye shughuli mbalimbali nk.

Anasema huduma nyingine wanazotoa ni uuzaji wa vimeng’enya (Bio-Enzymes) ambavyo mtu anaweza kuwe¬ka kwenye shimo la choo na matanki ya kuhifadhia maji taka na uchafu ukachakatwa kuwa maji ambayo yanawe¬za kutumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kumwa¬gilia kwenye bustani.

Vimeng’enya hivyo pia vinaweza kutumika katika mashino yanayopokea mizoga kwenye machinjio, mashino yanayopokea kondo la uzazi kwenye hospitali nk ili kurahisisha uchakataji wa taka.

CAPS Limited ndiyo kampuni ya kwanza nchini kuanzisha huduma ya ukodishaji vyoo na kutokana na uzoefu walionao katika utoaji wa huduma hizo wamekuwa wakifanya kazi katika shughuli mbalimbali za kitaifa.

Hii imetokana na kuwa na huduma na bidhaa bora kutoka kwa wazalishaji wanaotambulika duniani. Kampuni hiyo imepewa ithibati ya shirika la viwango duniani ISO 14001: 2015, ISO 45001: 2018, ISO 9001: 2015 kutoka TUV ya Austria

Marealle anasema kutokana na kufanya kazi katika viwan¬go vya kimataifa wamekuwa wakifanyiwa ukaguzi kila mwaka na wakaguzi wa ubora wa viwango wa nje wanaotambulika kimataifa.

Miongoni mwa tuzo hizo ni; tuzo ya kampuni inayotoa huduma bora Afrika Mashariki (2022) katika kundi la wafanyabiashara wadogo na wa kati, (SME’s), tuzo ya uuzaji bora wa jumla na rejareja (2023) inayotolewa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pakazi inayotolewa na OSHA, Tuzo ya Ubora kwa kampuni ndo¬go na za kati Tanzania iliyotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara na kuthibitihswa na TBS katika kampuni bora ya mwaka na mtoa huduma bora wa mwaka kwa miaka mitatu mfululizo (2021/2022, 2022/2023, na 2023/2024).

Akieleza kuhusu mafanikio hayo Marealle anasema yametokana na ushirikiano wa uongozi na wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao ndiyo msingi wa utendaji kazi wao pamoja na kuzingatia ubora.

“CAPS Limited tumekuwa tukizingatia viwango katika kila huduma na bidhaa tunayotoa kwa sababu tunafanya kazi na kampuni za kimataifa ambazo ubora kwao ni namba moja. Lakini pia ushirikiano mkubwa tulionao pamoja na kila mfanyakazi kutambua utamaduni wa kampuni na kuufuata,” anasema Marealle.

Akielezea kuhusu mikakati ya kampuni Marealle anas¬ema kwa sasa wanajipanga kufungua kitengo cha uzalish¬aji wa bidhaa za vimeng’enya (Enzymes) ambapo mpaka sasa wamefikia katika hatua nzuri.

“Upatikanaji wa vimeng’enya hivi kwa Watan¬zania utasaidia kupata bidhaa hizi kwa bei rahisi na ubora kwa sababu watakuwa hawa¬na shida ya kuagiza kutoka nje,” anahitimisha Marealle.

Kitalu # 103, Kinondoni Cattages, Brabara ya Binti Matola,

kama unaelekea Brabara ya Tunisia, Ada Estate.

S.L.P 13574, Dar es Salaam, Tanzania

Simu: +255 22 2668995, Nukushi: +255 22 2664145

Simu ya Mkononi +255 71 3606 644/+255 78 7606 644

Simu ya Mezani: +255 75 3664 466

Baruapepe: admin@caps. co.tz |Tovuti: www.caps. co.tz