Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amewaomba Watanzania waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, marehemu William Lukuvi aliyefariki Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma.
Akiongea kwa niaba ya Serikali nyumbani kwa marehemu Area D, jijini Dodoma leo, Alhamisi, Machi 26, 2026, Waziri Mkuu amesema: “Kwa niaba ya Serikali natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa. Jambo hili zito, gumu kulielewa, gumu kulipokea.”
…Lakini ndio limeshatufika na sote hatukutarajia maana Mheshimiwa Waziri alikuwa kazini. Tuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu na kuifariji familia. Mwenyezi Mungu awaimarishe kwa sababu yeyé ndio mfariji mkuu,” amesisitiza.