Nyota wa zamani wa Man United, Rio Ferdinand akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kwa ziara yake ya siku nne nchini.
Ferdinand amepokelewa na Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda na maofisa wengine wa serikali na wadau wa michezo pamoja na umati mkubwa wa mashabiki.