Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Ghana, John Mahama baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Arusha leo Jumatatu, Machi 2, 2025.
Rais Mahama amewasili jijini Arusha kwa ajili ya ziara ya kikazi, ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mwaka mpya wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, na sherehe za kumbukizi ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Mahakama hiyo mwaka 2006.