Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais, Samia Suluhu Hassan aKIwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati akitokea nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na kupokewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi leo Ijumaa Februari 6, 2026.
Rais Samia ametoka Dubai kushiriki Mkutano wa Dunia wa Serikali (World Governments Summit – WGS) 2026 pamoja na uzinduzi wa Jukwaa la Kimataifa wa Uwekezaji Afrika (GAIS).