Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Uganda leo Jumanne Mei 12, 2026 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za uapisho wa Rais mteule wa nchi hiyo, Yoweri Museveni.
Samia amepokewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe na Naibu Waziri Mkuu wa Tatu wa Uganda, Rukia Isaya Nakadama baada ya kuwasili nchini humo.