Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameshiriki Dua maalum ya kumuombea aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume ikiwa ni miaka 54 tangu kuuawa kwake.
Dua hiyo maalumu imefanyika Ofisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kisiwandui, Zanzibar leo Jumanne Aprili 7, 2026.
Viongozi mbalimbali wameshiriki akiwemo, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, Wazir Mkuu wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.