Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, Addis Ababa nchini Ethiopia leo Februari 14, 2025 kwa ajili ya kushiriki mkutano wa kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU). Pamoja na mambo mengine pia Samia atashiriki mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika.