Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Sadhia Abdallah (wa pili kulia) Doreen Mshana wa kwanza (kulia), Wilson Tarimo ( wa pili kushoto) tarehe 31 Oktoba 2024, mjini Iowa, nchini Marekani.
Vijana hawa watatu ni manusura wa ajali ya basi la Shule ya Msingi Lucky Vincent iliyotokea Mei 6, 2017 katika eneo la Rothia wilayani Karatu mkaoni Arusha. Vijana hao wapo nchini Marekani wakiendelea na masomo ya elimu ya juu katika vyuo vikuu tofauti.