Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameondoa nchini kwenda Urusi kwa ziara ya Kitaifa itakayoanza kesho Jumatano, Juni 2-5, 2026 kwa mualiko wa Rais wa Urusi, Vladimir Putin.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam leo Jumanne, Juni 2, 2026, Rais Samia ameagana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila na Mkuu wa Majeshi (CDF), John Mkunda.