Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Biashara wa Jimbo la Shandong, Wang Lei, kwa lengo la kujadili masuala ya kimkakati na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika, Alhamisi Machi 19, 2026, viongozi hao walijikita katika kuhamasisha uwekezaji kati ya Tanzania na Jimbo la Shandong nchini China, wakilenga zaidi sekta muhimu za maendeleo.