Licha ya kutofanyika sherehe za kuadhimisha miaka 62 ya Mapinduzi Zanzibar, vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama vimeadhimisha siku hiyo kwa kufanya matembezi maalumu na mazoezi ya kawaida kuweka mwili katika hali ya utayari.
Majeshi hayo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Vikosi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), wameahidi kuendelea kushirikiana kuhakikisha amani na utulivu vinadumishwa kama yalivyokuwa malengo ya Mapinduzi.
Matembezi hayo ya kilomita nane yaliyojumuisha majeshi sita, yameanzia Mtoni hadi viwanja vya Mnazimmoja Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Zanzibar.