Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) imeleta mabasi mapya 49 yatakayoongeza nguvu katika barabara ya Kimara, Dar es Salaam.
Mabasi hayo kwa sasa yapo katika karakana ya kampuni hiyo eneo la Ubungo, yakifanyiwa maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kutoa huduma rasmi Januari hii.