Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche, wakati akizungumza katika kongamano la wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu wanachama wa CHASO Mkoa wa Mwanza, ambapo amesisitiza umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu katika masuala ya uongozi, demokrasia na maendeleo ya taifa.
Katika kongamano hilo, Heche amewataka wanafunzi kutumia elimu yao kama nyenzo ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii na taifa kwa ujumla.