Mchezaji wa zamani wa Manchester United pamoja na timu ya taifa ya England, Rio Ferdinand, leo Mei 21, 2026 ametembelea hifadhi ya taifa ya Serengeti na kushuhudia maajabu ya uhamaji wa nyumbu katika hifadhi hiyo. Ziara ya Rio Ferdinand nchini Tanzania inahusisha shughuli za michezo na utalii, ambapo amepata nafasi, ya kutembelea bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania na kukutana na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Spika wa bunge pamoja waziri mkuu Dk Mwigulu Nchemba.