Mbunge wa Bunda Mjini mkoani Mara, Ester Bulaya akijumuika na waumini wa dini Kiislamu katika futari aliyowaandalia ikiwa na lengo la kuunga mkono ibada ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Futari hiyo iliyofanyika Jumamosi, Machi 14, 2026 imehudhuriwa na waumini na viongozi mbalimbali akiwemo Sheikh wa Wilaya ya Bunda, Abubakary Ally.