Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Emmanuel Nchimbi ameungana na viongozi pamoja na wananchi mbalimbali katika Adhimisho la Misa Takatifu ya kumbukizi ya miaka mitano ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania Hayati, Dk John Magufuli, inayofanyika leo Machi 17, 2026 Chato mkoani Geita.
Misa hiyo inaongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Rulenge – Ngara, Mhashamu Severine Niwemugizi.
Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021 ambapo leo imetimia miaka mitano tangu kifo chake huku akiacha alama katika siasa, uchumi, na utawala wa umma wa Tanzania.