Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Emmanuel Nchimbi ametoa maagizo kwa viongozi wa mikoa yote nchini kuhakikisha jitihada za upandaji miti zinaendelezwa kwa kuwekewa mkakati mahususi unaojumuisha makundi yote katika jamii.
Dk Nchimbi ametoa maelekezo hayo, wakati akifungua Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Siku ya Upandaji Miti Kitaifa, iliyofanyika mkoani Lindi, Alhamisi Machi 19, 2026.