Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ametaja mambo makuu matatu yanayokwamisha uchumi wa Zanzibar kukua kwa kasi na jinsi wanavyoyatafutia ufumbuzi yote kwa mpigo. Mambo hayo ni ufinyu wa bandari, uhaba wa umeme na hifadhi ndogo ya mafuta.
Dk Mwinyi ametoa kauli hiyo Jumapili Machi 22, 2026 wakati akihutubia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Bandari Jumuishi ya Mangapwani iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja ambayo itagharimu Dola za Marekani 300 milioni sawa na zaidi ya Sh770 bilioni.