Mbunge wa Bunda Mjini (CCM) Ester Bulaya, ametoa sadaka ya vyakula kwa ajili ya futari kwa waumini wa dini ya Kiislamu ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono ibada za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Sadaka ni sehemu pia ya kuimarisha mshikamano katika jamii, kama ambavyo Bulaya alivyoweka utaratibu katika kuwahudumia wananchi wa Bunda Mjini mkoani Mara.
Katibu wa mbunge huyo, Hussein Ruge amekabidhi msaada huo leo Alhamisi Machi 5, 2026, ambapo amesema sadaka hiyo imelenga kuwasaidia waumini wa Kiislamu kupata futari kwa urahisi katika kipindi hiki cha ibada takatifu.
Hata hivyo, Bulaya ameliambia Mwananchi sadaka ni endelevu kwa kuwa wananchi wa Bunda Mjini na amekuwa akifanya hivyo hata makanisani.