Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Januari 27, 2026, ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kushiriki shughuli ya upandaji miti katika eneo la Bungi Kilimo, Mkoa wa Kusini Unguja.
Photo: 1/4
Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Rosalynn Mndolwa-Mworia, amepanda mti kama ishara ya kuthibitisha dhamira ya kampuni hiyo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kulinda mazingira na kuleta mchango chanya kwa jamii, sambamba na Mwongozo wa Athari za Kijamii wa MCL (Social Impact Framework).
Photo: 2/4
Waziri Mkuu wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amepanda mti mbele ya Ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma leo Jumanne, Januari 27, 2026 ikiwa ni kuunga mkono, uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake kwa kulinda mazingira.
Photo: 3/4
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Neema Nchemba akipanda mti mbele ya Ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma leo Jumanne, Januari 27, 2026 ikiwa ni kuunga mkono, uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake kwa kulinda mazingira.