Wachezaji Polisi Tanzania wapata ajali, mmoja avunjika miguu

Muktasari:
- Kikosi cha timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara kimepata ajali leo Ijumaa Julai 9, 2021 wakati kikitoka mazoezini katika Uwanja wa TPC.
Kikosi cha timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara kimepata ajali leo Ijumaa Julai 9, 2021 wakati kikitoka mazoezini katika Uwanja wa TPC.
Makamu mwenyekiti wa timu hiyo, Robert Munisi amesema,”kwa sasa ni mapema kuwa na taarifa ya nini kilitokea lakini kwa kifupi gari liliacha njia na kugonga mti, hivyo kwa haraka walioumia ni zaidi ya wachezaji 10 na Mathias Mdau amevunjika miguu yote miwili.”
"Dereva wetu amevunjika mbavu moja, ndio taarifa za awali ninazoweza kukueleza lakini bado naendelea kufuatilia hapa KCMC walipokuwa majeruhi na kisha nitatoa majibu kamili ya kilichotokea.”
Polisi Tanzania inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 42 na ilikuwa inajiandaa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliopangwa kuchezwa wiki ijayo katika Uwanja wa Ushirika Moshi.