Vigogo Ulaya uso kwa uso
Muktasari:
- Man City ilifanikiwa kufuzu kwenye kwenye hatua hiyo baada ya kuichapa Club Brugge mabao 3-1 na kumaliza katika nafasi ya 22 iliyowapeleka kwenye mtoano.
London, England. Manchester City inatakiwa kuweka maombi mbele ili isipangwe na Real Madrid kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kesho, huku Arsenal ikitarajiwa kukutana na vigingi.
Droo ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora na mtoano inatarajiwa kupangwa kesho, ambapo timu nane zimeshafuzu moja kwa moja, huku nyingine 16 zikicheza hatua ya mtoano ili kupata nyingine nane ambazo zitafuzu kwenye hatua hiyo muhimu.
Timu nane zilizofuzu moja kwa moja baada ya michezo ya jana ni Liverpool, Barcelona, Arsenal, Inter Milan, Atletico Madrid, Bayern Leverkusen, Lille na Aston Villa.
Wakati hizo zikiwa zimefuzu, timu 16 ambazo zitacheza mtoano ni Atalanta, Borussia Dortmund, Real Madrid, Bayern München, Milan, PSV , Paris Saint-Germain, Benfica, Monaco, Brest, Feyenoord, Juventus, Celtic, Manchester City, Sporting CP na Club Brugge.
Man City ilifanikiwa kufuzu kwenye kwenye hatua hiyo baada ya kuichapa Club Brugge mabao 3-1 na kumaliza katika nafasi ya 22 iliyowapeleka kwenye mtoano.
Sasa timu hiyo ambayo ilitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2023, hatua ya mtoano inaweza kupambana na aidha Real Madrid au Bayern Munich kwenye droo itakayopangwa kesho.
Kama City, itakutana na Madrid itakuwa ni mechi ya kisasi kwa kuwa mabingwa hao wa kihistoria wa Ulaya walifanikiwa kuitupa nje miezi 12 iliyopita ambapo kama City ikifuzu ina maana kuwa timu zote nne za England zitakuwa zimekwenda 16 bora zikiwemo Liverpool, Arsenal na Aston Villa.
Hata hivyo, kama City itafuzu kwenda 16 bora inatarajiwa kukutana na aidha Bayer Leverkusen au Atletico Madrid.
Liverpool ambayo ilipoteza mchezo mmoja tu kati ya minane na kumaliza kileleni kwenye msimamo ikiwa bora zaidi ya timu 36 zilizoshiriki hatua hiyo inaonekana kukutana na timu mchekea kwenye hatua droo inayopangwa leo.
Vijana hao wa kocha Arne Slots, wanatarajiwa kupangwa na aidha Monaco, Brest, PSG au Benfica kwenye hatua ya 16 bora ikionekana kuwa na wapinzani wasio na nguvu sana kwenye michuano hii mikubwa Ulaya.
Arsenal ambayo imeonekana nayo kufanya vizuri kwenye michuano ya msimu huu, baada ya kumaliza nafasi ya tatu pointi sawa na Barcelona iliyomaliza ya pili nayo inatarajiwa kukutana na vigogo kati ya AC Milan, Juventus, PSV na Feyenoord.
Arsenal chini ya Mikel Arteta haina timu kibonde kutokana na timu zote hizo kuonyesha kiwango cha juu kwenye michuano hii msimu huu.
Barcelona ambayo ilifanikiwa kuonyesha kiwango kizuri kwenye michuano hii inatarajiwa kupangwa kati ya PSG, Benfica, Monaco au Brest, huku Inter Milan ambayo imefuzu ikiwa nafasi ya nne inaweza kukutana na na timu mojawapo kutokana nchini kwao aidha AC Milan au Juventus nyingine ni PSV Eindhoven au Feyenoord.
Kwa upande wa Aston Villa ambao wameonyesha kiwango bora kwenye michuano hii baada ya kupata nafasi ya kufuzu 16 bora kwa kuichapa Celtic mabao 4-2 jana yenyewe inaweza kupangwa na Atalanta, Borussia Dortmund, Sporting Lisbon au Club Bruges .
Timu zinavyoweza kupangwa kwenye hatua ya mtoano:
Atlanta: Sporting Lisbon au Club Brugge
Borussia Dortmund: Sporting Lisbon au Club Brugge
Real Madrid: Celtic au Man City
Bayern Munich: Celtic au Man City
AC Milan: Feyenoord au Juventus
PSV: Feyenoord au Juventus
PSG: Monaco au Brest
Benfica: Monaco au Brest
Feyenoord: AC Milan au PSV
Juventus: AC Milan au PSV
Celtic: Bayern Munich au Real Madrid
Manchester City: Bayern Munich au Real Madrid
Sporting Lisbon: Atalanta au Borussia Dortmund
Club Brugge: Atalanta au Borussia Dortmund.
Timu zinaweza kukutana hivi hatua ya 16 Bora
Liverpool: PSG, Benfica, Monaco au Brest
Barcelona: PSG, Benfica, Monaco au Brest
Arsenal: AC Milan, PSV Eindhoven, Feyenoord au Juventus
Inter Milan: AC Milan, PSV Eindhoven, Feyenoord au Juventus
Atletico Madrid: Real Madrid, Bayern Munich, Celtic au Man City
Bayer Leverkusen: Real Madrid, Bayern Munich, Celtic au Man City
Lille: Atalanta, Borussia Dortmund, Sporting Lisbon au Club Brugge
Aston Villa: Atalanta, Borussia Dortmund, Sporting Lisbon au Club Brugge.