Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uwanja mpya wa Manchester United utakuwa hivi

Muonekano wa uwanja mpya  wa Manchester United utakavyokuwa, utajengwa pembeni ya uwanja wa Old Trafford.

Muktasari:

  • Uwanja huo umebuniwa na mbunifu maarufu England, Lord Norman Foster, ambaye ameufanya kuwa wa kipekee zaidi duniani.

Manchester, England. Manchester United imepanga kujenga Uwanja mpya ambao utakuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 100,000 tofauti na wa sasa unaobeba mashabiki 74,310.

Muonekano wa nje ya uwanja mpya wa Manchester United ukionyesha njia iliyopewa jina la Wembley iliyopambwa na miti kuelekea uwanjani. Picha na mtandao

Uwanja huo wa kisasa utakuwa na minara mitatu mikubwa kama ilivyo kwenye nembo ya timu hiyo. Minara hiyo itabeba mwamvuli mkubwa wa kioo ambao utafunika sehemu ya Uwanja kuhakikisha mashabiki wanakaa kwenye mazingira yasiyoathiriwa na mvua.

Muonekano wa uwanja mpya wa Manchester United utakavyokuwa wakati wa usiku. Picha na mtandao

Uwanja huo mpya utajengwa pembeni kidogo na ulipo uwanja wa sasa wa Old Trafford ambao umetumika kwa miaka 115, United imepanga kugharamia ujenzi wa uwanja huo kwa Dola 2. 996 bilioni (Sh6 trilioni).

Muonekano wa uwanja mpya wa Manchester United wenye muundo wa kisasa. Picha na mtandao