Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Trump awafungia mashabiki Kombe la Dunia

Los Angeles, Marekani. Kombe la Dunia la 2026, limeanza kukumbwa vikwazo baada ya mashabiki kutoka mataifa 15 yanayoshiriki mashindano hayo kufungiwa maombi yao ya viza na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitoa waraka wa ndani siku ya Jumatano unaowaelekeza maafisa wa ubalozi kukataa maombi ya viza kutoka nchi 75 tofauti, wakati idara hiyo inapitia upya taratibu za uchunguzi na uhakiki wa waombaji.

Kati ya nchi hizo 75, mataifa 15 yanatarajiwa kushiriki Kombe la Dunia la msimu huu litakalofanyika nchini Marekani, Mexico na Canada ikiwemo moja ya timu zinazopigiwa upatu zaidi, Brazil.

Jambo la kushangaza, timu tatu kati ya nne zilizopo kwenye Kundi C la Scotland zimeathiriwa na mgogoro huu wa viza, huku Brazil, Morocco na Haiti zote zikiwa kwenye orodha nyekundu ya Trump.

Hali hiyo inaweza kusababisha viwanja visijazwe mashabiki katika mechi zote za hatua ya makundi za Scotland, ambapo michezo itachezwa Foxborough (dhidi ya Haiti na Morocco) na Miami (dhidi ya Brazil).

Mataifa mengine yaliyoathiriwa na mpango huu wa kushtua ni Algeria, Cape Verde, Colombia, Ivory Coast, Misri, Ghana, Iran, Jordan, Senegal, Tunisia, Uruguay na Uzbekistan.

Idara ya Mambo ya Nje inatarajiwa kuanza utekelezaji wa kusitisha kwa muda usiojulikana utoaji wa viza kuanzia Januari 21. Gazeti la Daily Mail limewasiliana naShirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ili kupata ufafanuzi zaidi kuhusu jinsi mashabiki wa mataifa hayo watakavyoathiriwa.

Waraka uliotumwa juzi unaelekeza maafisa wa ubalozi kukataa maombi ya viza kutoka kwa waombaji watakaohitaji kutegemea misaada ya kijamii mara watakapoingia Marekani.

Maafisa pia wameagizwa kuzingatia vigezo mbalimbali kwa waombaji, vikiwemo afya, umri, na uwezo wa kuzungumza Kiingereza.

“Mamlaka ya muda mrefu ya Idara ya Mambo ya Nje itatumika kuwatangaza kuwa hawastahiki wahamiaji wanaoweza kuwa mzigo wa kijamii kwa Marekani na kutumia vibaya ukarimu wa wananchi wa Marekani,” alisema msemaji wa Idara ya Mambo ya Nje, Tommy Piggott.

“Uhamiaji kutoka nchi hizi 75 utasitishwa wakati Idara ya Mambo ya Nje inapofanya tathmini upya ya taratibu za uchakataji wa uhamiaji ili kuzuia kuingia kwa raia wa kigeni watakaotegemea misaada ya kijamii.”

Idara ya Mambo ya Nje itatoa misamaha kwa baadhi ya maombi, lakini imesisitiza kuwa itakuwa kwa kiwango “kidogo sana.”

Hatua hii inakuja wakati Trump akitafakari jinsi ya kuchukua hatua dhidi ya Iran kufuatia maandamano ya kitaifa hivi karibuni.


Mataifa yaliyoathiriwa na marufuku ya Trump

Brazil

Morocco

Haiti

Algeria

Cape Verde

Colombia

Ivory Coast

Misri

Ghana

Iran

Jordan

Senegal

Tunisia

Uruguay

Uzbekistan.