Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simeone afichua sababu ya kubadili hoteli London

Muktasari:

  • Arsenal itavaana na Atletico katika mechi ya marudiano ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayofanyika kwenye Uwanja wa Emirates.

London, England. Meneja wa Atletico Madrid, Diego Simeone, amesema uamuzi wa timu yake kubadili hoteli kuelekea katika mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal leo, haukuwa wa kishirikina bali ni gharama nafuu za hoteli hiyo.

Oktoba mwaka jana Atletico walifikia katika hoteli ya nyota nne ya Marriott kabla ya kipigo cha mabao 4-0 walichopata dhidi ya Arsenal, lakini safari hii wamehamia hoteli ya nyota tano ya Courthouse iliyopo Shoreditch, mashariki mwa London kwa ajili ya mchezo wa marudiano uliosalia baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza.

Akizungumzia mabadiliko hayo, Simeone amesema kwa utani kuwa sababu kubwa ilikuwa ni gharama nafuu ya hoteli hiyo, akipuuza tetesi kuwa walikuwa wanajaribu kuondoa mkosi wa matokeo mabaya ya awali.

Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone wakati akizungumza na vyombo vya habari kuelekea katika nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal. Picha na Mtandao

“Hoteli ilikuwa nafuu zaidi, ndiyo maana tulibadilisha,” amesema Simeone.

Wakati huo huo, Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta, amewataka wachezaji wake kuingia uwanjani kwa nguvu kubwa na kucheza kwa bidii ili kufuzu fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20.

“Kitu pekee ninachotaka ni kukamilisha maandalizi kwa kiwango cha juu kabisa, na timu iende uwanjani kama wanyama, ifurahie wakati huo na ipambane kwa nguvu zote.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta wakati akizungumza na vyombo vya habari kuelekea katika nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico. Picha na Mtandao

Nendeni mkachukue nafasi hiyo. Unapokuwa karibu na fursa kama hii, ina maana uko tayari kuitumia. Na timu itaingia kuanzia dakika ya kwanza kupambana na kupata ushindi,” amesema Arteta.

Arteta amesema kikosi chake kinapaswa kutumia vizuri nafasi hiyo muhimu, akisisitiza kuwa huu ni wakati wa kihistoria kwa klabu hiyo inayosaka tiketi ya kufika fainali kwa mara ya pili tangu walipofanya hivyo 2006.

Katika taarifa nyingine njema kwa Arsenal, nyota Martin Odegaard na Kai Havertz wamethibitishwa kurejea kikosini kuelekea mchezo huo. Hata hivyo, mlinzi Jurrien Timber ataendelea kukosekana kutokana na majeraha.