Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yachezea kichapo mbele ya Rais Magufuli

Rais wa Tanzania, John Magufuli akiwa jukwaani katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Saalam akishuhudia mtanange baina ya Yanga SC dhidi ya Simba SC.

Muktasari:

  • Mara ya mwisho Rais Magufuli alipokuwa uwanjani hapo alishuhudia Simba ikipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar msimu wa 2017/18.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli kwa mara ya pili anaishuhudia Simba ikifungwa bao 1-0 na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Rais Magufuli ni shabiki wa Simba aliingia uwanjani hapo saa 10:40 jioni ikiwa ni muda mchache baada ya Rais wa CAF, Ahmed Ahmed kuingia uwanjani hapo.

Rais Magufuli alikuwa amevaa jezi yake ambayo nusu ilikuwa na rangi ya Yanga na upande mwingine rangi nyekundu huku akiwa amevaa kofia yenye rangi ya bendera ya Tanzania.

Leo Rais Magufuli akiwa amekaa jukwaani na mgeni wake rais wa CAF, Ahmed alishuhudia Simba ikipokea kipigo kingine cha bao 1-0 kutoka kwa watani zao wa jadi.

Mshambuliaji Bernard Morrison alifunga bao pekee la Yanga kwa mpira wa adhabu katika dakika 44 na kuhamsha shangwe kwa mashabiki uwanjani hapo.

Bao hilo lilimfanya Rais Magufuli kufurahi na kuwapungia mashabiki wa Yanga waliolipuka kwa shangwe kubwa baada ya bao hilo.

Mara ya mwisho Rais Magufuli alipokuwa uwanjani hapo alishuhudia Simba ikipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar msimu wa 2017/18.

Baada ya mchezo huo Rais Magufuli wakati akiikabidhi Simba ubingwa msimu 2017/18, alisema Kagera Sugar ikitoboa tundu na kuongeza kusema kwa mpira huu unaocheza hamuwezi kuchukua ubingwa wa Afrika.